Red_arrow

Ungependa kuifanya Kiswahili kuwa lugha ya chaguo lako, katika tovuti hii? |

Muungano wa vyama vya Djibouti vyafanya mikutano ya uchaguzi

Februari 12, 2013

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Muungano wa vyama vitatu vya kisiasa nchini Djibouti vilifanya mikutano ya uchaguzi Jumapili na Jumatatu (tarehe 10 na 11 Februari), kuelekea kwenye chaguzi za wabunge zilizopangwa kufanyika tarehe 22 Februari.

Muungano wa upinzani wa Union for National Salvation (USN), ambao hapo zamani ulikuwa ukijulikana kama Holy Union for Change, ulifanya uchaguzi katika mji wa Balbala siku ya Jumapili, ukiongozwa na Ismail Gedi Hared, liliripoti Shirika la Habari la Djibouti. Huku wakizungukwa na wafuasi waliovaa rangi ya machungwa, wagombea wa USC walikariri shauku yao ya kuwepo kwa uchaguzi wa huru na haki. "Wakati wa wakubwa wanaokatalia mamlaka umekwisha na matakwa ya watu inapaswa kusimamia mabadiliko,' Hared alisema.

Pia siku ya Jumapili, llyas Moussa Dawaleh, kiongozi wa muungano wa chama kinachotawala cha Union for a Presidential Majority (UMP), aliwatangaza wagombea kwa wafuasi wa muungano huo waliokuwa wamevalia mavazi ya kijani karibu na uwanja wa Gouled, liliripoti gazeti la La Nation la Djibouti. Viongozi wa UMP waliwaomba wananchi wa Djibouti wasighiribiwe na ahadi za vyama vya upinzani. "Kutokana na sera zilizoundwa na Rais Ismail (Guelleh) na vyama ambavyo vinaunda muungano huu, nchi yetu sasa inaendelea, inapitia mageuzi na inajijenga yenyewe, na pia mustakabali wake wa baadaye una nuru", alisema Hassa Said Goumaneh, mmoja kati ya wagombea wakuu wa UPM.

Chama cha kisiasa za mrengo wa kati cha Centre for Unified Democrats (CDU) kilikutana na wafuasi wake katika uwanja wa Manispaa wa Falah Had siku ya Jumatatu, kikiongozwa na Omar Elmi Khaireh. Khaireh alitoa wito kwa wafuasi hao kupiga kura kwenye uchaguzi ujao, huku akibainisha changamoto za utawala wa sasa ikiwemo rushwa ambayo imetawala serikalini, upendeleo wa kindugu na upendeleo kwa jumla, ambayo alisema kuwa yote yanakwamisha maendeleo yakiuchumi ya Djibouti.

Kampeni za uchaguzi zilifunguliwa Ijumaa tarehe 8 Februari na zitaendelea kwa muda wa wiki mbili. Huu ni uchaguzi wa kwanza wa Djibouti ambao hautumii mfumo wa kushiriki vyama vikubwa pekee katika utawala, na unatarajiwa kutoa haki kwa vyama vidogo kuwa na sauti kubwa katika serikali.

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, jinsi gani watu walio ughaibuni wanaweza kuisaidia vizuri zaidi Somalia?

Angalia matokeo