Jela za Tanzania zimejaa wafungwa wenye makosa madogo

Januari 22, 2013

  • 1 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Kamati ya bunge iliyopewa jukumu la kuchunguza hali ya jela za Tanzania iligundua kwamba asilimia 90 ya wafungwa ni vijana wasiokuwa na ajira wanaokabiliwa na makosa madogo madogo, alisema mwenyekiti wa kamati hiyo Edward Lowassa siku ya Jumatatu (tarehe 21 Januari).

Lowassa alitetea matumizi ya utawala wa mwendelezo wa kesi kutatua kesi za wafungwa kwa wakati, liliripoti gazeti la The Guardian la Tanzania. "Idara hizi lazima ziimarishe kazi zao na zishirikiane badala ya kila idara kufanya kazi peke yake na matokeo yake kuchelewesha kupitia umangimeza na ukosefu wa ufanisi," alisema.

Alisema ni hatari kwa nchi kuwafunga watu kwa makosa madogo madogo kwa vipindi virefu, hasa ikiwa asilimia 23 wanakabiliwa na kile alichokiita "kesi ndogo ndogo sana."

Kamati ya ulinzi, usalama na mambo ya nje ya bunge pia ilipigania fursa bora zaidi za habari kwa wafungwa na kurejeshwa kwa mfumo wa mahakama za watoto nchini Tanzania.

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • yusuph nindiro
    January 23, 2013 @ 09:56:21AM

    kweli kabisa watu wanaonewa ktk serikal ya Tz wakat wenye kes kubw wanaachiw tatiz kubwa ni rushwa tu amna lengine

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, jinsi gani watu walio ughaibuni wanaweza kuisaidia vizuri zaidi Somalia?

Angalia matokeo