Mapigano mapya Tana River Delta yaua 39

Desemba 21, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Kiasi cha watu 39 waliuawa katika mapigano mapya kati ya jamii za Pokomo na Orma katika eneo la Tana River Delta hapo Ijumaa (tarehe 21 Disemba), liliripoti shirika la habari la AFP.

Jamii hizo mbili zilipigana hivi karibuni katika majira ya kiangazi yaliyopita katika msururu wa uvamizi yalioua zaidi ya watu 100.

Ghasia za sasa zinaweza kuhusishwa na uchaguzi mkuu wa Kenya uliopangwa kufanyika mwezi Machi 2013, kwani mabadiliko ya mipaka ya wilaya yamepelekea kuondoka kwa nguvu za kisiasa kati ya makundi tafauti ya kikabila kwenye eneo hilo.

Polisi waliripotiwa kuiambia AFP kwamba mkasa huo wa hivi karibuni ulichangiwa na operesheni ya kuwanyang’anya watu silaha ambao ulishukiwa kulalia upande mmoja.

Picha zilizotumwa kwenye mtandao wa Twitter wa Msalaba Mwekundu zinaonesha viambaza vya mabanda yaliyovunjwa vikiwa vimesimama lakini mapaa yake yameteketezwa kabisa.

Shirika la Msalaba Mwekundu limesema kwamba timu lake la waokoaji lilikuwa likiwahudumia majeruhi, 30 kati yao wakiwa katika hali mbaya sana. Hawakutoa idadi kamili ya watu wote waliojeruhiwa.

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, jinsi gani watu walio ughaibuni wanaweza kuisaidia vizuri zaidi Somalia?

Angalia matokeo