Watu 323 wakamatwa kwenye msako wa usalama Mogadishu

Septemba 07, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Vikosi vya usalama vya Somalia viliwakamata watu 323, wengi wao vijana, katika operesheni ya usalama mjini Mogadishu hapo Alhamisi (tarehe 6 Septemba), uliripoti mtandao wa habari wa Somalia, Shabelle Media Network.

"Lengo la operesheni hiyo lilikuwa ni kuhakikisha usalama wa mji mkuu na kuyamaliza mabaki ya makundi ya wapinga amani mjini Mogadishu," alisema kamanda wa Usalama wa Taifa kwa mkoa wa Banadir Kanali Khalif Ahmed Ereg. Alisema maafisa wa polisi walisaidia katika operesheni hiyo, na vikosi hivyo viwili vitabakia kwenye hali ya tahadhari hadi usalama urudi mjini.

Operesheni hiyo ilikuwa ukamataji mkubwa kabisa wa watu wengi kuwahi kufanywa na Usalama wa Taifa ukiwalenga watuhumiwa wa al-Shabaab na makundi yenye silaha yanayotishia amani, liliripoti shirika hilo la habari.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 2)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, katiba ya Kenya inapaswa kurekebishwa ili kulipa baraza jipya la Seneti madaraka zaidi?

Angalia matokeo