Septemba 07, 2012
Sharmarke Abdi, mwenye umri wa miaka 18, na Said Omar, umri miaka 24, walijisalimisha kwa utawala wa mkoa wa Puntalnd hapo Alhamisi (tarehe 6 Septemba) baada ya kutoroka kutoka milima ya Galgala, maficho ya al-Shabaab.
"Hivi karibuni, wote maafisa na wanajeshi wamekuwa wakijisalimisha kwa utawala walipong'amua kwamba wanadhoofika katika mikoa ya kusini mwa nchi kwa sababu ya kupoteza ngome zao," Naibu Waziri wa Usalama Abdi Jamal Osman Mohamed aliiambia Sabahi.
Alisema kuwashikilia vijana hawa kwa muda mrefu katika maeneo ya milima kumehatarisha mustakabali wao.
"Ukubalifu wa mawakala wa usalama kwa uasi wa watu hawa unafuatia utekelezwaji wa msamaha wa kirais wa Puntland kwa vijana wanaoondoka al-Shabaab, ukiacha majina makubwa yaliyotajwa na jumuiya ya kimataifa," alisema Mohamed.
Vijana hao waliopotoshwa walisema walikuako kwenye milima ya Galgala kwa miezi 13, alisema. Utawala wa Puntland uliwaonesha vijana hao wawili kwa vyombo vya habari siku ya Alhamisi.
Polisi nchini Tanzania walimkamata mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msingwa, na wafanyabiashara 60 k...
Mahakama moja ya Bosaso iliwatia hatiani na kuwapiga faini Wairani 78 siku ya Jumapili (tarehe 19...
Polisi nchini Tanzania waliwakamata watuhumiwa 15 kuhusiana na kulichoma Kanisa la Bethania kweny...
Mkuu wa Polisi wa Kenya, David Kimaiyo, ameondoa nafasi za afisa polisi wa jimbo, afisa wa upelel...
Watu wenye silaha waliwaua watu wawili na kuwajeruhi wengine wanne katika mashambulizi tofauti kw...
Mkutano wa kuzungumzia uwezekano wa uchimbaji mafuta na gesi, uwekezaji, usalama na miundombinu n...
Wizara ya Masuala ya Wanawake na Familia ya Puntland ilianza mafunzo ya siku nane hapo Juampili (...
Zaidi ya Wasomali milioni 1 hawatakuwa na "usalama wa chakula" hadi mwezi wa Septemba, Mtandao wa...
Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Pembe ya Afrika (IGAD) uliwatembelea maafisa mjini Mogadish...
Mshukiwa wa ugaidi na mke wake walipigwa risasi na kufa na maafisa sita wa polisi walijeruhiwa wa...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Vijana waliobakia wanapaswa kufuata mfano huu MZURI na kujisalimisha kabla KDF haijawakamata.