Red_arrow

Ungependa kuifanya Kiswahili kuwa lugha ya chaguo lako, katika tovuti hii? |

Tanzania kupanua matumizi ya teknolojia ya nyuklia ili kusimamia ubora wa chakula

Agosti 28, 2012

  • 1 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Mamlaka ya Chakula na Madawa Tanzania (TFDA) imepanua matumizi ya teknolojia ya nyuklia ili kusimamia na kuboresha usalama wa chakula nchini, gazeti la Tanzania la The Citizen liliripoti.

TFDA imeweka kifaa maalumu cha maabara ili kugundua na kuchambua viharibifu vya metali, mabaki ya dawa zaa kuulia wadudu na vijisumu katika mazao ya chakula.

"Tunaatekeleza mkakati kazi wetu mpya wa miaka mitano kutoka 2012 hadi 2017," alisema Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hitti Sillo katika uzinduzi wa mpango huo huko Dar es Salaam siku ya Jumapili (tarehe 26 Agosti). "Miongoni mwa malengo ya mpango huu ni kuipatia vifaa maabara ili kuchambua dawa za mifugo na mabaki ya dawa za kuulia wadudu ifikapo mwezi Juni 2015."

Mpango huu unasaidiwa na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki, ambalo lilitoa shilingi milioni 345 million shillings (dola 220,000) kwa mradi huu, pamoja na vifaa vya maabara vyenye thamani ya kiasi cha shiilingi milioni 86 (dola 55,000).

Kaimu afisa mkuu wa afya Donald Mmbando alisema awamu ya kwanza wa mpango wa ulinzi wa chakula kwa kutumia nyuklia, ulioanza mwaka 2007 hadi 2010 iliongeza usalama wa chakula Tanzania, kwa vile bidhaa za chakula kilichoagizwa zilizoonekana kuwa na vichafuzi na vijisumu vilikataliwa kuingia nchini.

"Kusimamia vyakula vinavyoingia katika masoko yetu ni kitu ambacho hakiwezi kudharauliwa katika ulimwengu wa leo. ambao umekuwa kama kijiji cha dunia kukiwa na mzunguko huru wa bidhaa," alisema.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 2)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • lugendo.R.H
    August 29, 2012 @ 07:14:12AM

    UKIANGALIA THAMANI YA VIFAA TULIOPEWA MSAADA NA SHIRIKA LA ATOMIKI SERIKALI INAUWEZO WA KUGALAMIA,ILA 2MEISHA ZOEA MISAADA KUTOKA NJE.TUNASHUKURU ILA ISIWE KWA KUWA WAMEGUNDUA URANIAM KWETU WAKAANZA KU2NYONYA.WAJALI MASLAHI YA WANANCHI

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo