Wafadhili wa kimataifa kufadhili mtambo wa umeme wa upepo na kiwanda cha kusafisha maji Djibouti

Agosti 28, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Djibouti inapanga kujenga kiwanda cha kuzalisha umeme wa upepo chenye thamani ya faranga bilioni 18 (dola milioni 100) na kiwanda cha kusafishia maji katika bandari ya Doraleh, liliripoti gazeti la La Nation la Djibouti hapo Jumatatu (tarehe 27 Agosti).

Kiwanda hicho cha maji kitatoa ujazo wa mita 45,000 za maji safi kila siku, na utafiti unatabiri kwamba kinu cha umeme wa upepo kitatoa megawati 20 kwa siku.

Mradi huo unakusudiwa kumaliza upungufu wa maji ya kunywa nchini humo, hasa kwa wakaazi 820,000 wa mji mkuu. Serikali inatarajia kinu cha umeme wa upepo kupunguza gharama za kusafishia maji, na kuruhusu utoaji wa maji kwa gharama nafuu kwa watumiaji.

Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Ulaya umeahidi msaada wa faranga bilioni 4.4 (dola milioni 25) kwa mradi huo na Shirika la Maendeleo la Pembe ya Afrika (IGAD) limeahidi msaada wa kati ya faranga bilioni 6.6 na bilioni 9.9 (kati ya dola milioni 38 na milioni 56) wa Djibouti chini ya mpango wake wa nishati endelevu.

Serikali ya Djibouti itafanya jitihada za kupatikana kwa sehemu iliyobakia ya fedha hizo, liliripoti gazeti hilo rasmi la serikali.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 1)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo

Nyenzo