Agosti 27, 2012
Askari wa Umoja wa Afrika na wa Somalia waliuteka mji muhimu wa bahari wa Marka kutoka kwa wanamgambo wa al-Shabaab wenye mafungamano na al-Qaida siku ya Jumatatu (tarehe 27 Agosti), maafisa walisema.
"Tumeichukua Marka; tuliingia pamoja na vikosi vya serikali ya Somalia asubuhi hii," alisema Kanali Ali Aden Hamud, msemaji wa Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia.
"Kulikuwa na mapigano kidogo, lakin sio mazito sana; askari wengi wa al-Shabaab walikimbia," alisema, kwa mujibu wa AFP.
Kuipoteza Marka, mji ulioko kilomita 70 kusini ya Mogadishu,ni pigo kubwa kwa al-Shabaab, ambayo imekumbwa na upotevu mkubwa wa kimkakati katika miezi ya karibuni. Marka ni mji wa nne mkuu kimkoa kukombolewa kutoka mikono ya al-Shabaab mwaka huu -- baada ya Beledweyne , Baidoa and na Hudur.
Kwa kushindwa huku karibuni, al-Shabaab wanashikilia udhibiti wa miji mikuu miwili ya bahari kusini ya Somalia -- Barawe na Kismayo -- ingawaje vikwazo vya majini ya kimataifa vimebana sana kufikiwa huko kwa njia ya bahari.
Polisi nchini Tanzania walimkamata mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msingwa, na wafanyabiashara 60 k...
Mahakama moja ya Bosaso iliwatia hatiani na kuwapiga faini Wairani 78 siku ya Jumapili (tarehe 19...
Polisi nchini Tanzania waliwakamata watuhumiwa 15 kuhusiana na kulichoma Kanisa la Bethania kweny...
Mkuu wa Polisi wa Kenya, David Kimaiyo, ameondoa nafasi za afisa polisi wa jimbo, afisa wa upelel...
Watu wenye silaha waliwaua watu wawili na kuwajeruhi wengine wanne katika mashambulizi tofauti kw...
Mkutano wa kuzungumzia uwezekano wa uchimbaji mafuta na gesi, uwekezaji, usalama na miundombinu n...
Wizara ya Masuala ya Wanawake na Familia ya Puntland ilianza mafunzo ya siku nane hapo Juampili (...
Zaidi ya Wasomali milioni 1 hawatakuwa na "usalama wa chakula" hadi mwezi wa Septemba, Mtandao wa...
Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Pembe ya Afrika (IGAD) uliwatembelea maafisa mjini Mogadish...
Mshukiwa wa ugaidi na mke wake walipigwa risasi na kufa na maafisa sita wa polisi walijeruhiwa wa...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Wasomali lazima wawe huru kutoka kwa magaidi washenzi wa al-Shabaab.
Haja ya kudhibiti ugaidi imeongezeka, na kuiharakisha serikali ya Somalia na washirika wake wa Magharibi kuchukua hatua kali za pamoja. La wazi zaidi, hatua hizi ni pamoja na kuweka vizuizi kwa vijana wanaotembelea Somalia kwa lengo la kujiunga na vikundi vya ugaidi, au wanaotaka kujaribu kuendesha mafunzo katika kambi za magaidi. Kwa kuongezea, hatua nyengine ni pamoja na kuitupia jicho jumuiya ya Wasomali walioko Uingereza, pamoja na kusimamia mawasiliano baina ya watu ili kufichua ukiukwaji wowote mkubwa unaoweza kuwasaidia magaidi kutekeleza njama zao kwa ufanisi. Pia, serikali ya Somalia sasa inajihusisha kwa nguvu na vita dhidi ya ugaidi kupitia kuidhishwa kwa katiba mpya, ambayo imekusudiwa kuwa kiini cha mchakato mzuri wa kisiasa nchini Somalia. Katiba pia ni mwangaza wa uhuru wa kusema na mfumo wa wengi wa kitaalamu. Badala yake, mabadiliko haya yatasaidia kuandaa mazingira yanayofaa kwa kutokomeza ugaidi. Kwa upande mwengine, changamoto kubwa ya maharamia walio na kambi salama kwenye mwambao wa Somalia ambao wanahatarisha shughuli za baharini katika Bahari ya Arabuni. Maharamia pia wanatoa tishio kwa meli za mafuta zinazoelekea Marekani na Ulaya. Matokeo yake, kumekuwepo na ushirikiano unaozaa matunda baina ya serikali ya Somalia na wenzake wa Ghuba ya Arabuni, Marekani na Ufaransa ili kutafuta suluhisho litakalosaidia kutokomeza suala hili la uharamia, ambalo bado linahatarisha usalama wa eneo hili hadi leo.