Agosti 19, 2012
Wizara ya Elimu ya Juu ya Kenya iliidhinisha siku ya Ijumaa (tarehe 17 Agosti) shule tano za mafunzo ya polisi ya diploma, gazeti la The Standard la Kenya liliripoti.
Fursa zilizopanuliwa kwa elimu ya polisi nchini Kenya ni sehemu ya jitihada za Kamati ya Utekelezaji wa Mabadiliko ya Polisi kuboresha huduma kwa umma, na zitatolewa huko Kiganjo, Embakasi, Utawala, Emali na Nairobi. Programu zitakuwa wazi kwa maofisa wa polisi waliopo na raia waliohitimu.
Kupitia makubaliano na Chuo Kikuu cha Kenyatta, Chuo cha Polisi cha Kenya kitatoa elimu ya kuwawezesha maofisa kuongeza sifa za taaluma zao, ambazo kabla ya hapo walizilitafuta nje ya jeshi kwa gharama zao.
Kamati ya polisi pia hivi karibuni iliwasilisha mtaala mpya kwa ajili ya mafunzo ya polisi ambayo yanalenga haki za kibinadamu, jinsia, mawasiliano na uhusiano na umma, maadili na miiko, huduma na kumjali mteja.
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) alitoa majina mawili ya mwisho ya ...
Watu watano waliuawa na wanne kujeruhiwa katika mashambulizi mawili kwenye eneo la kaskazini mash...
Sababu kuu ya vurugu ambazo ziliua zaidi ya watu 150 katika Delta ya Mto Tana mwaka jana ilitokan...
Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza mlipuko wa polio katika Pembe ya Afrika siku ya Jumatan...
Majeshi ya serikali ya Somalia yamezifungia kampuni za mawasiliano ya simu na biashara nyingine h...
Serikali ya Somalia itaanza kuunda tawala za kikanda katika maeneo yaliyokombolewa kutoka kwa al-...
Waziri wa Nishati wa Djibouti Ali Yacoub Mohamoud na Balozi wa Japani nchini Djibouti Atsushi Nis...
Ufunguzi wa Mkutano wa Wasambazaji wa mafuta na gesi Tanzania utafanyika huko Dar es Salaam tareh...
Wabunge wameondoa hoja yao inayomtaka Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon na baraza lake la mawaziri k...
Rais Ahmed Silanyo wa mkoa wa Somaliland alikutana na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya kwa Som...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Oooh Polisi wa Kenya. Kwa vyovyote vile, hili ni jeshi ambalo limejaa aibu kwa ufisadi sugu. Ni aibu...Aibu....Aibu...Polisi anapewa sare ya buluu kwa utambulisho rahisi wa kujipatia shilingi 50 kwa nguvu. Katika safari zangu husikia kichefuchefu ninapoona kundi la maofisa wa polisi katika vizuizi vya barabarani wakibadilishana mikono ya ufisadi na waendesha magari. Kuna tofauti ndogo baina ya polisi hawa wa vizuizi vya barabarani na al-Shabaab wa Somalia. Operesheni Linda Nchi malizeni kazi yenu haraka mje kuanzisha Operesheni Linda Nchi wamalize kazi yao kwa haraka na waingie kwa operesheni Linada wenye magari dhidi ya al-Shabaab hawa katika vizuizi vya barabarani zetu ili kuifanya trafiki yetu iwe ya kistaarabu.