Umoja wa Afrika watuma salamu za Idd kwa Wasomali

Agosti 19, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Mwakilishi Maalumu wa Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika ya Somalia, Balozi Boubacar Diarra alituma salamu za Idd kwa watu wa Somalia siku ya Jumapili (tarehe 18 Agosti 18th).

"Idd al-Fitr ya mwaka huu imekuja katika kipindi muhimu kwa historia ya Somalia, kwa sababu nchi hivi karibuni ilipitisha katiba ambayo ilimaliza miaka 12 ya serikali za mpito na inajiandaa kuikaribisha serikali mpya baada ya miongo kadhaa ya vurugu,"alisema Diarra, kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Somalia.

Diarra pia alitoa shukrani zake na salamu za Idd kwa wanajeshi wanaotumikia Jeshi la Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM). "Kufanya kwenu kazi kwa bidii na kujitolea kumeipa Somalia fursa nzuri iliyokuwa nayo katika miongo mingi kupata amani na utulivu," alisema.

AMISOM inaendelea kuahidi kuisaidia Somalia, na itaendelea kufanya kazi pamoja na serikali mpya iliyoanzishwa baada ya madaraka ya Serikali ya Mpito ya Shirikisho kumalizika siku ya Jumatatu, alisema.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 2)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo