Somalia yataja majina ya wabunge 202 kabla ya siku ya mwisho Jumatatu

Agosti 19, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Kamati ya Utaalamu ya Uteuzi ya Somalia (TSC) imetaja majina ya wabunge wapya 202 siku ya Jumamosi (tarehe 18 Agosti), AFP liliripoti.

"Tuna wabunge 202 waliyo tayari sasa na tunashughulikia kuchunguza wengine 40 ambao wamepitishwa leo," alisema Mwenyekiti mwenza wa Kamati Halimo Yarey. Bunge linatarajiwa kuchagua Rais mpya wa Somalia Jumatatu, siku ya mwisho ya madaraka ya Serikali ya Mpito ya Shirikisho, iwapo akidi ya wabunge 184 itafikiwa.

Mwishoni bunge litakuwa na wabunge 275. "Orodha iliyobakia bado inasubiri kwa sababu ya mabishano ndani ya koo na sababu nyingine zinazohusiana na kutotimizwa kwa masharti," Yarey alisema.

Kamati inachagua wabunge kutoka katika orodha iliyotolewa na viongozi 135 wa kikabila kutoka nchi nzima. Takriban wagombea 70 wameondolewa kwa kushindwa kutimiza masharti ya kutumikia bunge, kama vile diploma ya sekondari na kutokuwa na uhusiano na mabwana wa vita.

Katika kiasi kilichotengwa cha 4.5 , bunge litakuwa na wabunge 61 kutoka katika kila moja kati ya koo nne kuu za Somalia -- Darod, Dir, Hawiye na Rahanweyn -- na wengine 31 kutoka katika muungano wa vikundi vya walio wachache.

Mkoa wa Puntland wa serikali ya Somalia ulitoa kauli Jumamosi ukishutumu kuingiliwa kwa kazi ya TSC .

"Tunatoa wito kwa pande zote husika kuheshimu kutopendelea upande wowote, uhuru na uamuzi wa TSC," taarifa hiyo ilisema, ikiuunga mkono kamati kwa kazi yake hadi sasa.

Naye Rais wa Kenya Mwai Kibaki alisema katika taarifa yake Ijumaa kwamba waharibifu katika mchakato wa amani wa Somalia watakabiliwa na adhabu ya vikwazo kutoka katika serikali yake, Capital FM ya Kenya iliripoti.

"Tunapenda kutoa onyo la wazi kwa wale wote wanaokusudia kuharibu tena, kudhoofisha au kuchezea Mpango Mkuu kuelekea katika utulivu wa kudumu wa kisiasa baada ya Agosti 2012, kwamba Kenya haitavumilia vitendo hivyo," Kibaki alisema. Alisema usalama wa Somalia ni muhimu kwa ajili ya usalama wa Kenya na Afrika, akisisitiza msaada wa serikali yake kwa Somalia katika awamu inayofuata.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 5)

Dislike_icon(3)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo