Walinzi wa mwambao wa Djibouti wazuia wasafiri haramu 1,500 mwezi uliopita

Agosti 17, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Walinzi wa mwambao walizuia watu 1,500 wa uhamiaji haramu mwezi huu uliopita, kwa mujibu wa kamanda wa walinzi wa majini Luteni Kanali Waiss Omar Bogoreh.

"Hawa ni wengi sana kama utazingatia tangu kuanzishwa kwa taasisi hii, tumeshakamata jumla ya watu 4,000," Bogoreh alisema katika mahojiano na gazeti la Djibouti La Nation lililochapishwa (tarehe 16 Agosti). Jeshi la walinzi wa mwambao la Djibouti lilianzishwa kwa amri ya raisi mwaka 2010.

Bogoreh alisema kuwa pamoja na kupambana na biashara ya binadamu, walinzi wa mwambao wanafanyakzi kuzuia magendo haramu ya bidhaa na kuzuia uvuvi haramu nje ya mwambo wa nchi.

"Uchumi wa nchi yetu unategemea sana juu ya ukuaji wa shughuli za baharini na kwa hivyo walinzi wa majini lazima wawe tayari kukabiliana na mahitaji mapya katika kukua kwa safari zisizo za lazima," alisema.

Bogoreh alisifia juhudi za Djibouti za kupambana na uharamia katika kanda hii, kwa kusema kuwa nchi inafungamana na mipango ya kimataifa ya kuzuia uharamia katika Ghuba ya Adeni na Bahari ya Hindi.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo