Tasnia ya utalii Kenya kuimarika, waziri wa utalii asema

Agosti 17, 2012

  • 1 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Kenya inatarajia kupata shilingi bilioni 100 (dola bilioni 1.2) za mapato kutoka sekta ya utalii mwaka huu, Waziri wa Utalii wa Kenya Dan Mwazo alisema siku ya Alhamisi (tarehe 16 Agosti).

"Ikilinganishwa na mwaka jana ambapo nchi ilipata shilingi bilioni 98 (dola blioni 1.1) kutokana na utalii, mwaka huu tunatarajia kupata shilingi bilioni 100," Mwazo alisema wakati kwa kutembelea Mbuga ya Taifa ya Maasai Mara, gazeti la Kenya la The Standard liliripoti.

Ongezeko lingeweza kuwa kubwa zaidi kama sio kwa matokeo ya karibuni ya ugaidi nchini Kenya, Mwazo alisema.

Mwazo alisema alitarajia idadi ya watalii wanaokuja Kenya itaongezeka kwa sababu ya mkazo wa serikali katika kampeni za kuitangaza. "Tumefanikiwa kuitangaza kama mahali pazuri zaidi ulimwenguni pa mafikio ya watalii, lakini masuala ya usalama na mtandao mbaya wa barabara vimetishia kurejesha nyuma mapato yetu," alisema.

Aliongeza kuwa ongezeko la mapato yanaweza kupatikana kupitia juhudi za kupanua matangazo mbali zaidi ya masoko ya kawaida ya utalii ya Kenya ya Uingereza, Marekani, Ujerumani, Ufaransa na Asia. "Kutegemea kupita kiasi masoko ya kawaida hakutaongoza mapato ya utalii," alisema.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 2)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • حمد الناشي / الكويت
    June 3, 2013 @ 11:39:20PM

    Kwa bahati mbaya, Waafrika wa Kenya, wanataka fedha na utalii (bila ya kufanya kazi kwa bidii). Watalii wa nchi za Ghuba wanajali kuhusu usalama na usafi.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, katiba ya Kenya inapaswa kurekebishwa ili kulipa baraza jipya la Seneti madaraka zaidi?

Angalia matokeo