Agosti 17, 2012
Tanzania imeanzisha kifaa cha mtandaoni ili kuwasaidia wawekezaji na wajasiriamali kupata kwa urahisi habari za kisasa kuhusu taratibu zinazohusiana na uwekezaji, gazeti la Tanzania la Daily News liliripoti hapo Ijumaa (tarehe 17 Agosti).
Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) kwa sasa kinafuata mfumo huo unaojulikana kama "Taratibu za mtandaoni" (e-Regulations), kilichotengenezwa na Mkutano wa Umoja wa Mataifa juu ya Biashara na Maendeleo (UNCTAD).
"Wakati taratibu na hatua hizi zinazohusika zitakapojulikana na watu ungetarajia watu zaidi kuanza biashara na ongezeko la uwajibikaji katika kulipa kodi," alisema Kjartan Sorensen, meneja uwezeshaji biashara wa UNCTAD mwenye dhamana ya Taratibu za mtandaoni barani Afrika.
Kwa mujibu wa UNCTAD, taratibu za mtandaoni zinaweza kuchangia sana uwazi na ufanisi katika huduma za umma, kuimarisha uendeshaji na kupunguza gharama.
Ingawa mfumo huu uko katika benki ya data mtandaoni, wawekezaji na wajasiriamali wanaweza kupata habari za lazima za biashara, ikiwa ni pamoja na jinsi ya kuandikisha kampuni, kulipa kodi na kupata viza au cheti cha vichocheo katika TIC.
Wabunge wameondoa hoja yao inayomtaka Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon na baraza lake la mawaziri k...
Rais Ahmed Silanyo wa mkoa wa Somaliland alikutana na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya kwa Som...
Ukiritimba na ukosefu wa ufanisi katika bandari ya Dar es Salaam unaigharimu Tanzania na nchi jir...
Viongozi wa mkoa wa Puntland walikutana siku ya Jumanne (tarehe 21 Mei) kuwashajiisha wanawake ku...
Wanajeshi wa Somalia na wa Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) waliwakamata zaidi ...
Rais Ismail Omar Guelleh wa Djibouti alijadiliana ushirikiano wa kimkakati na Kanali Saleh Ben Na...
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, vikosi vya usalama na mahakama vinapaswa kuomba radhi hadharani kut...
Waziri Mkuu wa Djibouti Abdoulkader Kamil Mohamed alitoa wito wa kuongezwa kwa ushirikiano katika...
Baadhi ya wabunge wa Somalia wameitupilia mbali hoja ya kumtaka waziri mkuu na baraza lake la maw...
Wabunge wa upinzani walidai kwamba serikali ya Tanzania imekuwa ikibana uhuru wa kujieleza na kud...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji