Mahakama Kuu ya Kenya yawahukumu watuhumiwa wa Irani kubaki chini ya uangalizi

Agosti 17, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Mahakama Kuu ya Kenya ilihukumu siku ya Alhamisi (tarehe 16 Agosti) kwamba Wairani wawili wanaotuhumiwa kwa ugaidi ambao waliachiwa kwa dhamana mwezi uliopita watabakia chini ya uangalizi wa polisi hadi kesi zao zitakaposhughulikiwa, Star ya Kenya iliripoti.

Watuhumiwa hao wawili, Ahmed Mohamud na Sayed Mausud, walishitakiwa kwa kumiliki kilogramu 15 za mabomu yenye nguvu kubwa ya RDX katika maandalizi ya kufanya mashambulizi kwa Wakenya. Mwanasheria Lydia Achode alisema kukamatwa kulikuja baada ya taarifa za kuaminika zilizopendekeza kwamba kilogramu 100 za RDX zimesafirishwa kutoka Iran hadi Kenya, kilo 85 kati ya hizo hazikurejeshwa.

Mahakama hiyo Kuu ilibatilisha uamuzi wa mahakama ya chini wa kuwaachia watuhumiwa hao kwa dhamana ya shilingi milioni 2 (Dola za Kimarekeni 23,800) kwa kila mmoja mwezi uliopita.

Achode alisema Kenya haijasainiana na Iran mkataba wa watuhumiwa kuhukumiwa katika nchi waliyokosa (Kenya) na haieleweki kama watuhumiwa watarejea Kenya kwa ajili ya utekelezaji wao wa kurudi nchini kwao.

Alifuta madai yao kwamba walitakiwa kuachiwa huru kupata matibabu na kuona matunzo yaliyotolewa katika gereza yanatosheleza.

Kama watakutwa na makosa, Mohamud na Mausud watakuwa na uwezekano wa kufungwa gerezani.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 1)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo

Nyenzo