AMISOM yaomba ulinzi wa raia nchini Somalia

Agosti 17, 2012

  • 2 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

AMISOM itaendelea kutoa kipaumbele katika kuwalinda raia wa Somalia katika mgogoro wa kijeshi unaoendelea nchini Somalia, Mwakilishi Maalumu wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia Boubacar Diarra alisema Alhamisi (tarehe 16 Agosti).

"AMISOM inachukua jukumu lake kwa usalama wa wananchi wa Somalia kwa uzito mkubwa na inaelewa kikamilifu wajibu wake wa kuendesha operesheni bila ya kusababisha hatari kwa wananchi wenyeji," Diarra alisema.

Alisema wananchi wa Somalia ni muhimu katika mafanikio ya misheni ya AMISOM. Alionyesha "masikitiko makubwa" kuhusiana na ripoti za majeruhi wa kiraia huko Kismayo, akiongeza kwamba ripoti hizo zitachunguzwa.

Ripoti zilionya kwamba meli za kivita zilizotia nanga katika pwani ya Kismayo zilirushiana risasi na wapiganaji wa al-Shabaab katika mji Jumamosi, zikiwaua watu watatu na kujeruhi wanne.

"Tunaviomba vikosi vingine vya kijeshi kuweka vizuizi vinavyostahili katika maeneo yenye idadi kubwa ya raia," alisema.

Watumishi wa AMISOM wamekuwa wakifundishwa katika dhana ya sheria za binadamu za kimataifa na wana sera za kuwalinda wananchi, ikiwa ni pamoja na kutokuwa na kanda zisizo na moto katika maeneo yenye wananchi wengi, alisema, akiongeza kwamba jitihada za AMISOM kupunguza madhara kwa wananchi zimetambuliwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na mawakala wa kimataifa.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 2)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • muhammad
    August 21, 2012 @ 11:39:26PM

    Inafurahisha kuona kuwa dunia inajali kuhusu masuala ya Somalia, kwa sababu itawasaidia watu wa Somalia. Lakini haitakuwa na faida yoyote ikiwa Wasomali hawakushirikiana wao kwa wao ili kutatua matatizo yao. Ikiwa hawakuungana na kuwa na hamira ya kutatua mizozo yao ya ndani, jaribio lolote la kutatua suala hili kutoka nje litashindwa.

  • ongera
    August 21, 2012 @ 04:12:03AM

    Ninawaombea AMISOM WAFANYE KAZI KWA UMOJA ili kuleta kanuni katika Pembe ya Afrika. Watu wa SOMALIA LAZIMA WAKUBALI msaada wa nje uliopo ILI KULETA UTULIVU katika nchi yao.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo

Nyenzo