Jeshi la Kenya laua wapiganaji wa al-Shabaab 73

Agosti 17, 2012

  • 4 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Vikosi vya Ulinzi vya Kenya (KDF) viliwaua wapiganaji wa al-Shabaab 73 wakati wa mapambano katika mji wa Fatadun katika mkoa wa Gedo ulio kusini mwa Somalia Jumatano (tarehe 15 Agosti), Gazeti la Daily Nation la Kenya liliripoti.

Msemaji wa KDF Emmanuel Chirchir alithibitisha idadi hiyo katika mtandao wa Twitter, akisema vikosi vya Kenya viliteka zaidi ya AK-47 100.

Al-Shabaab pia walidai kuwa waliwaua zaidi ya wanachama 60 wa KDF na vikosi vya serikali ya Somalia.

Idadi ya waliokufa kwa pande zote mbili haikuweza kuthibitishwa kipekee.

Si chini ya askari wawili wa Kenya walijeruhiwa katika makabiliano hayo, ambayo yalianza wakati al-Shabaab waliposhambulia ngome za KDF huko Fafadun usiku wa Jumatano. Al-Shabaab walipanga kuvamia kambi hiyo, lakini vikosi vya KDF vilipata taarifa ya awali ya upelelezi na kusubiri mapambano, gazeti hilo liliripoti.

Askari waliojeruhiwa walichukuliwa kwa ndege hadi Nairobi kwa matibabu siku ya Alhamisi.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 19)

Dislike_icon(2)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • mawe
    August 19, 2012 @ 04:33:54PM

    KDF, shinikizeni na muwapiga. Tunawaunga mkono na tuko tayari kujitolea kwa dhamira hii yenye utukufu.

  • KEMBOI PHILEMON.
    August 19, 2012 @ 03:55:26AM

    HONGERA KWA KDF.

  • carol mwikali
    August 18, 2012 @ 02:51:04AM

    eventuary al-shabaab will be diffinted by the KDF/AMISOM.(kilicho na wanzo lazima kitakua na mwisho).

  • aden
    August 18, 2012 @ 01:48:04AM

    Nadhani ni kutojua kusoma au kuandika ndio uliowafanya wateseke.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo