Ungependa kuifanya Kiswahili kuwa lugha ya chaguo lako, katika tovuti hii? |
Agosti 10, 2012
Kenya inadhamiria kuwasilisha ombi la kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuwa mwenyeji wa Michezo ya Olimpiki 2024, liliripoti gazeti la Financial Times hapo Ijumaa (tarehe 10 Agosti).
"Kenya ilikuwa na imani hiyo tangu mwaka 1968 kufikiria kuandaa michezo ya Olimpiki," alisema Waziri Mkuu Raila Odinga akiwa jijini London. "Hiyo ni imani tunayohitaji kuwa nayo tena. Tunahitaji kuirudisha imani hiyo na tunaweza kufanya hivyo. Ni muhimu kuangalia nyuma kule tulikotoka na wapi tunataka kwenda, kwa sababu tumekuwa tukijikokota kwa muda mrefu mno," alisema.
Odinga alisema miundombinu na biashara ya Kenya itavuna "faida kubwa sana" kutokana na uwekezaji ambao ni lazima katika kuwa mwenyeji wa Olimpiki.
Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki imeelezea hamu yake ya kupokea maombi kutoka kwa nchi za Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara, kwa mujibu wa gazeti la Financial Times. Afrika ya Kusini, Qatar, Marekani, Morocco, Misri na Argentina zimetajwa kama wagombea katika kutayarisha Michezo ya 2024.
Polisi nchini Tanzania wamewakamata watu 90 siku moja baada ya maandamano ambapo mtu mmoja aliuaw...
Kenya ililiomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) kufutwa kw...
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia aliongoza sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa ...
Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa wanachama wa Shirika la Maendeleo la Pembe ya Afrika (IGAD) w...
Kiongozi wa jamii huko Zanzibar, Mohammad Omar Said, alishambuliwa kwa tindikali siku ya Alhamisi...
Mahakama moja ya Puntland imewahukumu kifo watu saba kwa mauaji ya ulamaa wa Kisomali, Abdulkadir...
Shirika la kimataifa la misaada la Global Partnership for Education (GPE) limetangaza msaada wa d...
Shirika la kimataifa la kuteteta haki za binadamu la Amnesty International limetoa wito kwa Kenya...
Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto ameahidi adhabu kali zaidi kwa majangili katika mswada wa Sh...
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) alitoa majina mawili ya mwisho ya ...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji