Jeshi la Somalia lafungua mahakama huko Balad

Agosti 10, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Jeshi la Somalia limefungua mahakama mpya huko Balad, Redio Bar-Kulan inayogharamiwa na Umoja wa Mataifa iliripoti siku ya ijumaa (tarehe 10 Agosti).

Hakimu Jenerali Hassan Mohamed Hussein aliongoza ufunguzi wa mahakama hiyo ambapo aliishukuru TFG na vikosi vya washirika kwa kuikomboa Balad kutoka kwa al-Shabaab na kufanya uanzishwaji wa mahakama kuwezekana.

Hussein alisema wanao watuhumiwa kadhaa wa wanamgambo wa al-Shabaab kizuizini, na baadhi yao tayari wamekubali kuwa wanachama wa kikundi cha mafungamano na al-Qaeda.

Hussein alisema atasimamia vizuri vikosi vya serikali ya Somalia huko Balad ili kuhakikisha heshima yao kwa wakazi wa eneo hilo, na kuwaonya dhidi ya kuendesha vituo haramu vya upekuzi, na kuongeza kuwa atawashitaki wale watakaovunja sheria.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 1)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo