Agosti 10, 2012
Polisi ya Kenya na Kamisheni ya Umoja wa Kitaifa na Maingiliano (NCIC) wameomba msaada wa wazee wa makabila kuepuka ghasia katika uchaguzi wa mwaka 2013, liliripoti gazeti la nchi hiyo la Daily Nation hapo Alhamis (tarehe 9 Agosti).
"Mazingira ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2013 ni tofauti na yale ya mwaka 2007. Sheria mpya imetupa mamlaka mengi na kila mtu atalazimika kukabiliana na sheria," alisema makamo wa msemaji wa polisi Charles Owino. "Hatutaki kusubiri hadi hatari zitokee na ndio maana tunajumuisha wazee wa jamii kama chanzo cha kutatua mizozo," alisema.
Juhudi za polisi zitaelekezwa zaidi katika majimbo 29 yaliyoainishwa kuwa ndiyo yanaweza kuwa "vyanzo moto" vya mizozo.
"Wakenya wa leo wana imani kubwa na polisi na tunaweza kulishughulikia hilo," Owino alisema. "Ukweli kwamba mkuu mpya wa polisi atakuwa huru kutojihusisha na mafungamano yoyote ya kisiasa hilo litafaa kwa kuongeza imani zaidi."
Kamati elekezi ya taifa ikiwa na wawakilishi kutoka polisi, Wizara ya Habari, Tume ya Mawasiliano ya Kenya, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka pamoja na NCIC pia zitasimamia vyombo vya habari na kuhamasisha kuimarisha umoja wa kitaifa.
Polisi nchini Tanzania walimkamata mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msingwa, na wafanyabiashara 60 k...
Mahakama moja ya Bosaso iliwatia hatiani na kuwapiga faini Wairani 78 siku ya Jumapili (tarehe 19...
Polisi nchini Tanzania waliwakamata watuhumiwa 15 kuhusiana na kulichoma Kanisa la Bethania kweny...
Mkuu wa Polisi wa Kenya, David Kimaiyo, ameondoa nafasi za afisa polisi wa jimbo, afisa wa upelel...
Watu wenye silaha waliwaua watu wawili na kuwajeruhi wengine wanne katika mashambulizi tofauti kw...
Mkutano wa kuzungumzia uwezekano wa uchimbaji mafuta na gesi, uwekezaji, usalama na miundombinu n...
Wizara ya Masuala ya Wanawake na Familia ya Puntland ilianza mafunzo ya siku nane hapo Juampili (...
Zaidi ya Wasomali milioni 1 hawatakuwa na "usalama wa chakula" hadi mwezi wa Septemba, Mtandao wa...
Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Pembe ya Afrika (IGAD) uliwatembelea maafisa mjini Mogadish...
Mshukiwa wa ugaidi na mke wake walipigwa risasi na kufa na maafisa sita wa polisi walijeruhiwa wa...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji