Reporters Without Borders waitaka Djibouti kumuachia mwandishi aliyefungwa jela

Agosti 10, 2012

  • 1 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Mwandishi wa habari Houssein Ahmed Farah alikamatwa nchini Djibouti hapo Alhamis (tarehe 9 Agosti), liliripoti shirika la kimataifa la kufuatilia uhuru wa habari, Reporters Without Borders (RSF).

"Mamlaka hazijatoa sababu yoyote ya kumkamata Farah na tunaitaka kumuachia mara moja," ilisema taarifa ya RSF. "Tuna wasiwasi sana na kuwekwa kwake kizuizini kwa kuwa ni mgonjwa wa sukari na anafunga Ramadhani. Ukichukulia hali ya hewa ya joto kali hivi sasa na mazingira magumu ya mahabusu nchini Djibouti, jambo hili linaweza kuwa na matokeo mabaya sana kwa afya yake."

Farah, mjumbe wa taasisi ya haki za binaadamu ya Djibouti iitwayo Djibouti Human Rights League and the Movement for Democratic Renewal and Development, amekamatwa mara kadhaa. Anaandikia mtandao wa habari wa upinzani, La Voix de Djibouti, iliyowahi kuwa redio na kugeuka kuwa mtandao wa habari ukiendeshwa na raia wa Djibouti wanaoishi uhamishoni Ulaya. Mtandao huo umezuia kupatikana ndani ya Djibouti lakini RSF imetengeneza njia inayowaruhusu raia wa nchi hiyo kuutumia.

Farah Abadid Hildid, mwandishi mwengine wa La Voix de Djibouti, anashikiliwa pia na polisi, kwa mujibu wa RSF.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 4)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • Mohamed Hassan
    August 10, 2012 @ 08:17:35PM

    Uchunguzi wa mwaka mzima ulionesha kuwa asilimia 50 ya viongozi wa Somaliland wanazo na wanazitumia paspoti za Jamhuri ya Djibouti. Maafisa wengi wa intelijensia, Mawaziri, Wabunge, viongozi wa kikabila. Waandishi wa habari na wafanyabiashara maarufu wa Somaliland wanatumia paspoti hii. Maafisa wa intelijensia wa Djibouti wanaotaka wasitajwe majina yao waliiambia Waagacusub kuwa pasipoti hizi huwa zinaongezwa muda mara mmoja kila baada ya miaka mitatu. Aliongeza kuwa raisi Ismael Omar Ghuelleh aliidhinisha kutolewa kwa pasipoti hizi, lakini alikataa kutoa maelezo zaidi. Vikundi vya upinzani vilieleza wasiwasi wao wa kuidhinishwa kwa paspoti hizi za Djibouti kwa raia wa Somalia wenye mafunagamano ya karibu ya kibiashara, kisiasa na kiintelijensia na Raisi Ghuelleh. Miongoni mwa wale wanaotumia pasipoti za Djibouti ni waziri wa mambo ya ndani wa Somaliland Mohamed Arraleh Nur aka Duurjaan, na msemaji wa raisi Abdullahi Ukuseh. Wawili hao wanaaminiwa kuwa ni wafanyakazi wa Idara ya Intelijensia ya Djibouti. Imegunduliwa kuwa yote haya yanafikiriwa na wengi kuwa ni mpango mpana wa Djibouti kuichukua Somaliland. Mhusika mkuu anayesimamia kuchukuliwa huku ni gavana wa Benki Kuu ya Djibouti Jama Hayd. Nyaraka zilizopatikana na Waagacusub.com zinaonesha kuwa gavana alilipa kiwango kikubwa cha fedha kwa mwenyekiti wa Baraza la wawakilishi la Somaliland Bw. Abdirahman Irroh, anayetoka kabila moja na mke wa raisi wa Djibouti. Zaidi ya hayo, Djibouti inaweza kuzuwia mawasiliano ya intaneti kwa watumiaji wenyeji nchini Somaliland.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo

Nyenzo