Waziri wa Ulinzi wa Somalia atangaza kunyang'anya silaha Mogadishu

Agosti 10, 2012

  • 1 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Serikali ya Somalia imeanza mpango wa usalama kwa kuwanyang'anya raia silaha na imepiga marufuku kubeba silaha mjini Mogadishu, iliripoti Redio Bar-Kulan inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa hapo Ijumaa (tarehe 10 Agosti).

Upigaji huo marufuku ni sehemu ya mkakati mkubwa wa kuongeza usalama katika mji huo kwa matayarisho ya uchaguzi wa uraisi hapo tarehe 20 Agosti, alisema Waziri wa Ulinzi, Hussein Arab Isse.

Isse aliwataka wakaazi wa Mogadishu kushirikiana na polisi na vikosi vya jeshi katika jitihada za kupunguza uhalifu na kuwapa taarifa panapokuwa na vitendo vinavyotilika mashaka.

Alisema wanasiasa wanahitaji kufanya kazi na vikosi vya usalama na aliwaonya kutokuizingiza kazi za kijeshi kwenye siasa.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 2)

Dislike_icon(1)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • Bashir
    August 12, 2012 @ 01:23:23PM

    Mogadishu ilikuwa muda mrefu iache bunduki chini. Silaha zisiwe katika mikono ya vikundi vya watu binafsi. Ninamlaumu raisi wa sasa kwa kukabidhi silaha nyingi kwa koo baada ya kuanguka kwa UIC. Laiti ungejua.[Illeen talo isuma kaa sheegto].

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo

Nyenzo