Agosti 10, 2012
Waziri Mkuu wa zamani wa Somalia, Mohamed Abdullahi Farmajo, alirejea Mogadishu hapo Alhamis (tarehe 9 Agosti), mwaka mmoja baada ya kujiuzulu wadhifa wake, kuzindua kampeni ya uraisi.
Wakaazi wa Mogadishu walikusanyika kwa kiwango kikubwa karibu na uwanja wa ndege wa Mogadishu na barabara ya Maka al-Mukarama kumkaribisha mgombea huyo wa uraisi.
Hata hivyo, majambazi wasiojulikana waliwashambulia waandamanaji kwa risasi, wakauwa watu wawili na kuwajeruhi wengine kadhaa katika eneo la Sayid Mohamed Abdullahi Hassan, karibu na jengo la bunge.
Farmajo amedai kufanyike uchunguzi kamili wa tukio hilo.
Mfuasi wa Farmajo aitwaye Siham Yunis, ambaye alikuwapo kwenye tukio, aliiambia Sabahi kwamba maandamano yalianza uwanja wa ndege na yalipokuwa yakikaribia mzunguko wa Sayid, watu wenye bunduki walirusha risasi kuelekea upande wao, wakaua na kuwajeruhi wafuasi kadhaa. Alisema baadhi ya wafuasi hao walifariki dunia wakati wakipelekwa hospitali.
Kufuatia mkasa huo, maafisa wa jeshi na usalama wa taifa walilifunga eneo hilo kwa lengo la kudhibiti hali.
Hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na kuwalenga waandamanaji, na hakuna yeyote hadi sasa aliyekwishakamatwa kwa kuhusishwa na tukio hilo. Baraza la Mawaziri la Somalia limeviamrisha vikosi vya usalama kuchunguza kadhia hiyo na kumaliza hujuma kama hizo zinazofanywa na makundi yenye silaha yanayotaka kuuzorotesha usalama kwenye mji mkuu.
Farmajo alikuwa waziri mkuu wa Somalia kutoka Oktoba 2010 hadi Juni 2011 alipojiuzulu kama sehemu ya Makubaliano ya Kampala yaliyoongeza muda wa serikali ya mpito hadi Agosti 2012.
Wabunge wameondoa hoja yao inayomtaka Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon na baraza lake la mawaziri k...
Rais Ahmed Silanyo wa mkoa wa Somaliland alikutana na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya kwa Som...
Ukiritimba na ukosefu wa ufanisi katika bandari ya Dar es Salaam unaigharimu Tanzania na nchi jir...
Viongozi wa mkoa wa Puntland walikutana siku ya Jumanne (tarehe 21 Mei) kuwashajiisha wanawake ku...
Wanajeshi wa Somalia na wa Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) waliwakamata zaidi ...
Rais Ismail Omar Guelleh wa Djibouti alijadiliana ushirikiano wa kimkakati na Kanali Saleh Ben Na...
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, vikosi vya usalama na mahakama vinapaswa kuomba radhi hadharani kut...
Waziri Mkuu wa Djibouti Abdoulkader Kamil Mohamed alitoa wito wa kuongezwa kwa ushirikiano katika...
Baadhi ya wabunge wa Somalia wameitupilia mbali hoja ya kumtaka waziri mkuu na baraza lake la maw...
Wabunge wa upinzani walidai kwamba serikali ya Tanzania imekuwa ikibana uhuru wa kujieleza na kud...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Habari hii sio sahihi kwa sababu wale waliowapiga watu risasi walikuwa majeshi ya Sheikh Sharif.