Kamati ya Ufundi ya Uteuzi ya Somalia yaongeza muda wa uchaguzi wa Bunge

Agosti 09, 2012

  • 2 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Kamati ya Ufundi na Uteuzi nchini Somali (TSC) imetangaza kuongeza muda wa kupokea wajumbe wapya wa Bunge hadi siku ya Alhamisi.

Kamati hiyo hapo awali ilipanga siku ya Jumatano kuwa muda wa mwisho wa kupokea orodha wa majina kutoka viongozi wa makabila 135 wanaokutana sasa mjini Mogadishu.

"Tumeamua kuwapa nafasi tena viongozi wa makabila ili watupatie wawakilishi wao waliobakia, haiyumkini kwetu kukutoruhusu uteuzi zaidi kwa viongozi wa makabila," alisema Abdullahi Osman mkuu wa TSC. "Haiwezekani kwetu kuwafungia milango viongozi wa makabila."

Kamati hiyo iliongeza muda wa masaa 24 kwa viongozi wa kikabila kuwasilisha wawakilishi wao, Osman aliiambia Sabahi. "Viongozi wa makabila walitakiwa kuwachagua wawakilishi wao kabla ya tarehe 5 Agosti, lakini hawakuweza kuitimiza tarehe hiyo na kisha wakashindwa tena kuuheshimu muda wa mwisho wa tarehe 18 Agosti. Sasa, hatuwezi kukubali tena kurudi nyuma," alisema.

Alisema kamati hiyo ya ufundi imeagiza viongozi wa kikabila kuzingatia muda huo wa mwisho ili kuharakisha hatua za uteuzi na kukamilisha orodha inayohitajika. "Hatuna muda wa ziada, na hatuwezi kusubiri zaidi," alisema.

Viongozi wengi wa kikabila wanasema hatua za uteuzi zinaendeshwa polepole kutokana na mkanganyiko kutoka kwa viongozi wa kisiasa na maafisa wa ngazi za juu wa serikali.

"Maafisa wa serikali wanajaribu kuwaathiri viongozi wa makabila kuteua wawakilishi wale watakaowapigia kura katika uchaguzi ujao," kiongozi wa kikabila, Ali Abdirahman, aliiambia Sabahi.

TSC ilitangaza wiki hii kwamba ilipokea majina kwa asilimia 70 ya wabunge wapya.

Osman alisema kamati hiyo itaanza kuzipitia rikodi za wagombea walioteuliwa kuthibitisha uhalali wake kwa mujibu wa kigezo vilivyowekwa na makubaliano ya Garowe.

TSC ina madaraka kamili za kufuta uteuzi wa mjumbe yeyote ambaye hajafikia vigezo vinavyotakiwa kwa wajumbe wa bunge, alisema. Vigezo hivi vinajumuisha mahitaji ya umri wa baina ya miaka 25 na 75, elimu ya chini ya sekondari na kutokuwa na rikodi ya uhalifu.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 2)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • Abdi hakim
    August 19, 2012 @ 11:04:21AM

    Wasomali wanataka amani wakati huu kwa hivyo mnapaswa kusalimu amri na kuja katika meza ya mazungumzo, wote al-Shabaab na Dmk, kitu kibaya zaidi ni kuwa watu wa dini na utamaduni mmoja wanapigana kwa miongo miwili iliyopita na hili limekuwa ni uharibifu mkubwa kwa nchi na watu wengi wameshamwaga damu yao bila ya kuangalia sifa za kuwa binadamu. Kitu cha mwisho sasa ni kuwa kamati ya uteuzi imeongezewa muda, ni aina gani ya mazingira inayowafanya wachelewe na wakati uliokubaliwa ni tarehe 20 kwa hivyo wanafanya nini? Utakuwa wakati wa uchaguzi huru na haki?

  • Abdi saciid xirsi
    August 12, 2012 @ 02:47:33AM

    Wasomali wamechoshwa na vita vya muda mrefu na uongozi mbaya. Kwa hivyo wawe na tahadhari kila kitu kinachoweza kusababisha uongozi mbaya, ukabila na kudharau sheria. Mbunge lazima awe mtunga sheria ambaye wakati huo huo anafuata sheria inavyotakikana.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo