Vikosi vya washirika vyapambana na al-Shabaab wilayani Hudur

Agosti 07, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Vikosi vya majeshi ya Somalia na Ethiopia viliwaua zaidi ya wanamgambo 30 wa al-Shabaab baada ya wanamgambo hao kukishambulia kituo chao huko Hudur hapo Jumatatu (tarehe 6 Agosti), iliripoti redio inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa ya Bar-Kulan.

Al-Shabaab walidai kwamba waliwaua zaidi ya wanajeshi 60 wa Ethiopia wakiwemo makamanda wanne wa ngazi za juu, kwa mujibu wa taarifa ya kundi hilo kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.

Idadi kamili ya walioathirika kutokana na tukio hilo haiwezi kuthibitishwa na vyanzo huru.

Mapigano hayo yalichukuwa masaa saba, alisema Mkuu wa Wilaya Mohamed Moalim Ahmed, yakiwajeruhi wanamgambo wengine 12. Hakusema chochote kuhusiana na hasara kwa upande wa vikosi vya washirika katika makabiliano hayo.

Haya ni mashambulizi ya pili dhidi ya vikosi vya Somalia wilayani Hudur tangu mwanzo wa Ramadhani. Vikosi vya washirika viliukamata mji huo kutoka mikononi mwa al-Shabaab mwezi Machi.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 4)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo