Mkuu wa wilaya ya Dadaab aukandamiza usafiri wa boda boda

Agosti 03, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Mkuu wa wilaya ya Dadaab Albert Kimathi ameapa kuwashughulikia waendesha teksi za pikipiki, maarufu kama boda boda, katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab, liliripoti gazeti la The Star la Kenya hapo Alhamisi (tarehe 2 Agosti).

Waendeshaji wa boda boda wamekuwa wakilaumiwa kwa kuwasafirisha wahalifu kuingia na kutoka kwenye kambi hiyo katika miezi ya karibuni. Tayari boda boda zimezuiwa kufanya kazi baada ya saa 12 jioni, alisema Kimathi.

"Tofauti na pale zamani ambapo tulikuwa na taksi tu, katika miezi ya hivi karibuni boda boda zimeibuka kama njia inayopendwa ya usafiri na wengi," alisema Kimathi. "Hii ndio sababu ya kutia shaka kwa sababu waendeshaji wake wanajilikana na wengi wao hawakusajiliwa. Tunahofu kwamba sasa wahalifu wanawatumia kufanya uhalifu wao."

Pikipiki mbili ziliwabeba washukiwa waliowateka wafanyakazi wa Baraza la Wakimbizi la Norwei mwezi uliopitakutoka kambi ya wakimbizi ya Ifo II na kuwapeleka Somalia, liliripoti gazeti hilo.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, katiba ya Kenya inapaswa kurekebishwa ili kulipa baraza jipya la Seneti madaraka zaidi?

Angalia matokeo