Rais wa Somalia atangaza msamaha kwa maharamia

Agosti 03, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Maharamia wanaweza kupatiwa msaada ikiwa watawaachia huru mateka wao na kurudisha vyombo walivyoviteka, alisema Rais Sheikh Sharif Sheikh Ahmed akizungumza na gazeti la London Times siku ya Ijumaa (tarehe 3 Agosti).

Baada ya kupiga kampeni zake mjini Balad, umbali wa kilomita 40 kaskazini mwa Mogadishu, Rais Ahmed alisema alikuwa tayari kurudia adhabu kwa maharamia 2,000 wanaofikiriwa kufanya shughuli zao katika pwani ya Somalia.

"Wale watakaoachana na kile walichokuwa wakifanya watasamehewa," alisema, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP. "Serikali itahakikisha kuwa milango iko wazi, ikiwa wanataka kuingia ndani."

Waziri Mkuu Abdiweli Mohamed Ali pia alionesha kuunga mkono kwake pendekezo hilo la msamaha. "Hakuna huruma kwa maharamia, sio kutoka kwangi, lakini kama wanaachana na kazi hiyo na kusema 'Ninatubu na naomba msamaha'; basi tunapaswa kufanya hivyo," alisema.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 1)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo