Barabara za Nairobi kufungwa kwa miezi sita

Julai 30, 2012

  • 2 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Mamlaka ya Barabara Kuu ya Kenya (KENHA) itafunga barabara kadhaa za Nairobi wakati wa ujenzi wa barabara mpya ya upande wa kusini wa mji huo, liliripoti gazeti la Kenya la Daily Nation siku ya Jumapili (tarehe 29 Julai).

KENHA itazifunga kabisa barabara za Community, Kibera na Nong, au kupunguza matumizi yake, kwa miezi sita ijayo, kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa KEHNA, Mishack Kidenda. Alisema waendesha vyombo vya maringi mawili watumie njia nyingine zilizowekwa kufikia barabara ya Lang'ata.

Barabara hizo zitafungwa kupisha ujenzi wa njia ya kusini mwa Nairobi, inayokusudiwa kupunguza msongomano katika mji mkuu huo.

Waziri wa Usafiri wa Haraka wa Nairobi, Jamlek Irungu Kamau alisema Nairobi imo kwenye mfululizo wa uimarishaji wa miundombinu yake. Miradi hiyo inajumuisha matengenezo ya barabara na uwekaji wa taa za mitaani katika baadhi ya masoko.

Benki ya Dunia imeikopesha Kenya dola milioni 600 (shilingi bilioni 50.5) kuimarisha huduma. Kiasi ya nusu ya fedha hizo zimetengwa kwa ajili ya Mradi wa Kuimarisha Usafiri wa Haraka wa Nairobi unaokusudiwa kuimarisha miundombinu katika mkoa huo wa mji mkuu.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 6)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • Jacob Njagi
    September 29, 2012 @ 05:01:05AM

    Hii ndio njia ya kuelekea Dira 2030. Wakenya wote tuunge mkono maendeleo haya bila ya kujali upande wao siasa/vyama. Hongera serikali.

  • Janet Wanjiku
    July 31, 2012 @ 01:44:54PM

    Ninathamini barabara za kando lakini nachukia usumbufu. Kazi lazima ifanywe kwa hivyo ujenzi wa barabara uanze.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, katiba ya Kenya inapaswa kurekebishwa ili kulipa baraza jipya la Seneti madaraka zaidi?

Angalia matokeo