Nchi 6 za Afrika Mashariki hatarini kwa upungufu wa chakula

Julai 30, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Mataifa sita ya Afrika Mashariki yako hatarini kuingia kwenye ukosefu mkubwa wa chakula huku watu wapatao milioni 16 wakiathirika katika kiwango kikubwa, kwa mujibu wa ripoti ya mwezi Julai ya Mtandao wa Kutoa Onyo la Ukame (FEWSN).

Onyo hilo la FEWSN linahusu nchi za Kenya, Djibouti, Ethiopia, Sudan, Sudan ya Kusini na Uganda, kunakosababishwa na upungufu wa mvua, migogoro, bei kubwa za chakula na baadhi ya wakati kutokuwa na uwezo wa kupata misaada ya kibinaadamu. Mtandao huo wa FEWSN ulioanzishwa na Shirika la Misaada ya Kimataifa la Marekani (USAID, linashirikiana na washirika wa kimataifa na wa eneo hilo kutoa taarifa za mapema za kuonya juu ya masuala ya usalama wa chakula.

Mvua katika maeneo ya kusini mashariki ya Kenya kutoka Machi hadi Mei zilikuwa za muda mfupi mwaka huu na maeneo ya kusini ya mkoa huo yanaweza kukifikia kiwango cha upungufu wa chakula, ilisema ripoti hiyo.

Msaada wa kibinaadamu wa chakula umefanya bei za chakula kutulia, pale hali ilipofikia kiwango cha njaa katika mwaka 2011. Hata baada ya kuimarishwa, bado zaidi ya asilimia 15 ya watu wanakabiliwa na kiwango kibaya cha utapiamlo katika maeneo kadhaa nchini humo.

Maeneo yanayotegemea kilimo kusini mwa Somalia, ikiwemo mikoa Bay, sehemu za Juba, Shabelle, Bakol na Gedo pia ilipata mvua za kiwango cha chini na zilizocholewa katika msimu wa mwaka huu wa mvua kuanzia Aprili hadi Juni, liliripoti shirika hilo.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 1)

Dislike_icon(1)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo

Nyenzo