Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania kupima uwezo wa kukabiliana na majanga baada ya ajali ya meli

Julai 30, 2012

  • 1 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Chama cha Msalaba Mwekundu cha Tanzania kitazindua programu ya kuwafundisha wafanyakazi wake wa kujitolea kuhusiana na matayarisho ya majanga, uokozi na huduma ya mwanzo, alisema Katibu Mkuu wa chama hicho alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

"Vile vile tunapanga kuliimarisha tawi letu la Zanzibar kuwa na uwezo wa kukabiliana na majanga kwa ufanisi wakati wowote yanapotokea," alisema Kimbisa, liliripoti gazeti la Tanzania la Daily News siku ya Jumatatu (tarehe 30 Julai).

Programu hiyo itafadhiliwa kwa shilingi milioni 10 (dola 6,300) zilizotolewa na mfanyabiashara Samantar Abdinur Iusuf, kwa kutambua mchango wa Chama cha Msalaba Mwekundu katika operesheni ya kuwaokoa wahanga wa ajali ya meli ya MV Star Gates iliyotokea kati ya Tanzania Bara na Zanzibar katikati ya mwezi huu.

Wafanyakazi 65 wa kujitolea na watatu wa kudumu waligawa mablanketi 200, mifuko 200 ya kuhifadhia maiti, glovu 200 na vifaa 200 vya kuvaa usoni wakati wa jitihada za uokozi.

Kimbisa alisema sehemu ya fedha hizo itatumika kununua vifaa vya uokozi na zilizobakia zitakwenda kwa wahanga wa ajali hiyo.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 1)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • Emmanuely Onesmo Lyimo
    October 29, 2012 @ 09:00:27AM

    Makala hii ni nzuri ila ni vyema sisi wanachama wa Redcross kuwe na utaratibu wa kukutana walau hata kwa mwaka mara tatu kwa lengo ya kukumbushana majukumu ya kazi na kama kuna tarifa mpya na mbinu nyingine za kisasa za huduma ya kwanza au uokoaji. Asante

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, katiba ya Kenya inapaswa kurekebishwa ili kulipa baraza jipya la Seneti madaraka zaidi?

Angalia matokeo