Bunge la Taifa la Katiba ya Somalia linaendelea licha ya shambulio la kombora

Julai 29, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Bunge la Taifa la Katiba ya Somalia (NCA) lilikutana tena siku ya Jumamosi (tarehe 28 Julai) baada ya mkutano wa Ijumaa kuahirishwa, gazeti la Somali la Garowe Online liliripoti.

Jengo lililokuwa chuo cha polisi ambamo NCA inakutana humo, lilifungwa kwa muda siku ya Ijumaa, baada ya makombora kadhaa kulipuka karibu na jengo hilo. Hakuna mtu aliyejeruhiwa katika milipuko hiyo.

"Kumaliza kupiga kura kwa ajili ya katiba ndio kikwazo tunachojaribu kukipambana nacho sasa, na huu ni mchakato muhimu ambao hauwezi kucheleweshwa," Waziri wa Somalia wa Katiba na Maridhiano Abdirahman Hosh Jibril alisema hapo Jumamosi. Alisema mkutano wa Ijumaa uliahirishwa kwa siku moja kutoka na sababu za kiufundi.

NCA, ambalo limepewa dhamana ya kuidhinisha rasimu ya katiba ya Somalia, lilifunguliwa mjini Mogadishu siku ya Jumatano baada ya kucheleweshwa kwa siku kadhaa . Usalama umezidishwa jijni ili kuzuia mashambulizi kutoka kwa al-Shabaab, ambayo imetishia kuwalenga wajumbe wa NCA.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 2)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo

Nyenzo