Julai 24, 2012
Viongozi na wadau wa Somalia wanapaswa kuheshimu muda wa mwisho uliowekwa kwa serikali ya kipindi cha mpito hapo tarehe 20 Agosti na wafanye kazi kwa ajili ya maslahi ya watu wa Somalia, limesema Baraza la Umoja wa Ulaya hapo siku ya Jumatatu (tarehe 23 Julai).
Baraza hilo lilipongeza makubaliano juu ya katiba ambayo wadhamini wa Mpango wa Amani wa Somalia jijini Nairobi mwezi uliopita, lakini likaeleza wasiwasi wake kwamba "kuendelea kusogezwa mbele na kukosekana kufikiwa kwa muda wa mwisho kunahatarisha uwazi na uhalali wa utaratibu wa kisiasa ulioanzishwa na Makubaliano ya Garowe ".
"Kuongezwa kwa muda wa taasisi za serikali ya mpito hakutakubalika na juhudi za kukwaza mageuzi halali nchini Somalia zitakabiliwa na hatua kali zinazostahiki," ilisema taarifa ya baraza hilo.
Umoja wa Ulaya "unautaka uongozi wa Somalia kufanya kazi kwa uwazi na kutoa taarifa kwa umma katika kipindi hiki kilichobakia," lilisema baraza hilo, likisisitiza umuhimu wa kutekeleza ahadi yake ya kuwa na asilimia 30 ya wanawake kwenye serikali ya shirikisho.
Baraza hilo liliwatolea wito wazee wa makabila nchini Somalia kukamilisha haraka uteuzi wa wajumbe wa Bunge la Katiba ili rasimu ya katiba iweze kuidhinishwa na kupigiwa kura ya maoni.
Mkutano wa Bunge la Katiba umeahirishwa mara kadhaalakini sasa umepangwa kufunguliwa mjini Mogadishu hapo siku ya Jumatano.
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) alitoa majina mawili ya mwisho ya ...
Watu watano waliuawa na wanne kujeruhiwa katika mashambulizi mawili kwenye eneo la kaskazini mash...
Sababu kuu ya vurugu ambazo ziliua zaidi ya watu 150 katika Delta ya Mto Tana mwaka jana ilitokan...
Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza mlipuko wa polio katika Pembe ya Afrika siku ya Jumatan...
Majeshi ya serikali ya Somalia yamezifungia kampuni za mawasiliano ya simu na biashara nyingine h...
Serikali ya Somalia itaanza kuunda tawala za kikanda katika maeneo yaliyokombolewa kutoka kwa al-...
Waziri wa Nishati wa Djibouti Ali Yacoub Mohamoud na Balozi wa Japani nchini Djibouti Atsushi Nis...
Ufunguzi wa Mkutano wa Wasambazaji wa mafuta na gesi Tanzania utafanyika huko Dar es Salaam tareh...
Wabunge wameondoa hoja yao inayomtaka Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon na baraza lake la mawaziri k...
Rais Ahmed Silanyo wa mkoa wa Somaliland alikutana na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya kwa Som...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji