Tanzania kuzalisha chakula cha ziada mwaka 2012

Julai 22, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Tanzania itazalisha zaidi ya chakula cha kutosha ili kukidhi mahitaji ya ndani mwaka huu, Waziri wa Tanzania wa Kilimo, Usalama wa Chakula na Ushirika Christopher Chiza aliliambia bunge siku ya Ijumaa (tarehe 20 Julai).

Zaidi ya tani milioni 13.5 za chakula zinatarajiwa kuvunwa mwaka huu, na kukidhi asilimia 113 ya mahitaji ya nchi, Chiza alisema, kwa mujibu wa gazeti la Tanzania la Daily News. Ziada kubwa katika mikoa nane itakidhi upungufu katika mikoa mengine sita, huku mikoa saba iliyobakia ikiwa inaweza kukidhi mahitaji yake yenyewe, alisema.

Chiza alisema sekta ya kilimo Tanzania ilichangia asilimia 23.7 ya uchumi wa nchi mwaka 2011. Uwekezaji mkubwa zaidi katika sekta hii unahitajika ili kufikia lengo la Mpango wa Taifa wa Maendeleo uliotarajiwa wa kiwango cha ukuaji wa asilimia 6, alisema, na kuongeza kuwa ukuaji katika sekta ya kilimo ulifikia asiliia 3.6 mwaka jana, na asilimia 4.2 mwaka 2010.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 1)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo

Nyenzo