Julai 22, 2012
Zamzam Mahmuud Farah na Mohamed Hassan Mohamed, wawakllishi wa Somalia katika Olimpiki , walipokewa na mashabiki mjini London siku ya Ijumaa (tarehe 20 Julai), Redio RBC ya Somalia iliripoti.
Wanachama wa Jumuiya ya Wasomali waliopo London walikutana na wanariadha katika kijiji cha Olympiki wakipeperusha bendera ya Somali na kuimba Wimbo wa Taifa.
"Leo nimefurahi sana kwa sababu sijawahi kufikiria ningekutana na wanariadha wa Somalia wakiwakilisha nchi yetu, lakini imetokea leo," Hafsa Farah Msomali anayeishi Uingereza mwenye umri wa miaka 19 alisema wakati wa sherehe ya ukaribisho.
Farah alisema michezo inaweza kusaidia kukabiliana na matatizo ya kisiasa nchini Somalia. "Michezo inaweza kuwaunganisha watu," alisema, kwa mujibu wa gazeti la Somalia Report. "Inaweza kuwa na nafasi kubwa katika kuunganisha jamii zinazopinzana."
Farah atakimbia katika mashindano ya mbio za meta 400, na Mohamed katika mashindano ya mbio za meta 1,500.
Polisi nchini Tanzania wamewakamata watu 90 siku moja baada ya maandamano ambapo mtu mmoja aliuaw...
Kenya ililiomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) kufutwa kw...
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia aliongoza sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa ...
Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa wanachama wa Shirika la Maendeleo la Pembe ya Afrika (IGAD) w...
Kiongozi wa jamii huko Zanzibar, Mohammad Omar Said, alishambuliwa kwa tindikali siku ya Alhamisi...
Mahakama moja ya Puntland imewahukumu kifo watu saba kwa mauaji ya ulamaa wa Kisomali, Abdulkadir...
Shirika la kimataifa la misaada la Global Partnership for Education (GPE) limetangaza msaada wa d...
Shirika la kimataifa la kuteteta haki za binadamu la Amnesty International limetoa wito kwa Kenya...
Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto ameahidi adhabu kali zaidi kwa majangili katika mswada wa Sh...
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) alitoa majina mawili ya mwisho ya ...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji