Mahakama ya Kenya yawaachia kwa dhamana washukiwa wawili wa ugaidi

Julai 17, 2012

  • 2 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Mahakama ya Kenya ilitoa dhamana kwa washukiwa wawili wa ugaidi wa Irani wanaoshitakiwa kufanya vitendo vya uharibifu mkubwa , Redio Capital FM ya Kenya iliripoti hapo Jumatatu (tarehe 16 Julai).

Washukiwa hao wawili, Ahmed Mohamud na Sayed Mausud, walishutumiwa kwa kumiliki kilo 15 za milipuko yenye nguvu ya RDX. Waliamriwa kusalimisha mahakamani pasipoti zao na kutakiwa kuripoti kwa kitengo cha Polisi wa Kupamabana na Ugaidi mara mbili kwa wiki.

"Nimebaini kuwa wawili hawa si wafanyaji wa makosa makubwa na hata kama ndio hivyo, katiba inawaruhusu kupewa dhamana, Jaji Mkuu Paul Biwott alisema. Dhamana hiyo ilipangwa kuwa shilingi milioni 2 (dola 23,000) kwa kila mmoja.

Polisi ya Kenya iliomba dhamana hiyo ikataliwe , kwa kusisitiza kuwa washukiwa hao wawili walikuwa tishio kwa usalama.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • benson
    September 9, 2012 @ 06:57:15AM

    Kenya ni eneo la ufisadi halmuradi tu uwe nacho, una haki ya kutenda kupita uwezo wa sheria.

  • حكيم المصري
    July 17, 2012 @ 06:48:20PM

    Hii inaonyesha wazi kuenea sana kwa ufisadi ndani ya Mahakama ya Kenya. Kwa kutumia pesa, unaweza kukodi chumba cha Kibaki na kumtoa nje. Zaidi, karibuni mtasikia kuwa watu wawili hawa wamekimbia nchi kwa kughushi pasipoti, na kesi itafungwa. Ni huzuni kwenu, watumwa wa dirham na dinari.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo