Mashambulio ya maharamia yapungua katika bahari ya Somalia

Julai 17, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Mashambulio ya maharamia yalipungua katika nusu ya kwanza ya 2012 kwa vile vikosi vya majini vya kimataifa vinavyofanya doria nje ya bahari ya Somalia vimechukua juhudi za kuwazuia maharamia wasiteke meli, Ofisi ya Bahari ya Kimataifa (IMB) ilitangaza hapo Jumatatu (tarehe 16 Julai).

Mkurugenzi wa Mapambano dhidi ya Maharamia wa Puntland Abdirizak Mohamed Dirir alisema kuwa Kikosi cha Polisi cha Majini cha Puntland kilikuwa na jukumu kubwa katika kupunguza uharamia katika eneo hilo.

"Ripoti ya [IMB] ni kweli, lakini haikutaja juhudi za kipekee za Puntland katika mapambano haya," Dirir aliiambia Sabahi.

Mambo mengi yamechangia katika kupunguza uharamia, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa usalama katika meli, na juhudi za vikoso vya majini vya kikanda na Umoja wa Ulaya katika kupambana na uharamia.

"Naamini kuwa juhudi za vikosi vya Puntland ni kipengele kikubwa kilichochangia katika kupunguza uharamia," Dirir alisema. Vimefanya operesheni katika mwambao za kanda hii, vimekata njia ya kujipatia vitu kwa maharamia na vimewakamata maharamia wengi."

Dirir alisisitiza umuhimu wa kuwalenga maharamia wakiwa katika ardhini pamoja na baharini, na alisema Puntland inahitaji fedha zaidi za kuunga mkono hatua hizi.

"Katika mikutano [kadhaa], tumekuwa tukisema mara kwa mara kuwa operesheni za vita dhidi ya uharamia ardhini lazima ziimarishwe, hata hivyo jumuiya ya kimataifa bado haijafikia huko," alisema.

Mwezi uliopita, Raisi wa Somali Sheikh Sharif Sheikh Ahmed aliomba silaha na nyenzo ili kupambana na uharamia , kwa kusema kuwa nchi yake inaweza kumaliza uharamia ndani ya mwaka mmoja.

Misheni mpya ya Umoja wa nchi za Ulaya dhidi ya uharamia

Umoja wa nchi za Ulaya (EU) hapo Jumatatu (tarehe 16 Julai) ilitangaza kuanzisha misheni mpya ya kiraia, EUCAP Nestor, kupambana na uharamia katika pembe ya Arika, kwa mujibu wa taarifa ya EU.

Misheni hii mpya ina lengo la kuimarisha uwezo unaoendelea katika kanda na kuvifunza vikosi vya polisi wa mwambao na majaji nchini Somalia.

"Kwa kuanzisha misheni hii mpya katika Pembe ya Afrika, EU unaonesha kwa mara nyingine tena wajibu wake wa vita dhidi ya uharamia," alisema Mwakilishi wa EU Catherine Ashton. "Chini ya uongozi wa nchi wenyewe, natumai kuwa EUCAP Nestor itatoa ufumbuzi wa mwisho katika kumaliza uharamia."

Timu ya kiasi cha watu 175 kitapelekwa katika kusimamia bahari nje ya Djibouti, Kenya, Ushelisheli na Somalia, ambazo zimekubali msaada uliotolewa na EU.

Misheni hiyo itapelekwa hadi Tanzania karibuni inavyowezekana, EU ulisema

Katika hotuba yake bungeni, Waziri wa Ulinzi na Ujenzi wa Taifa Shamsi Vuai Nahodha alielezea juhudi za jeshi la Tanzania dhidi ya uharamia.

Alisema meli moja tu imetekwa nyara mwaka huu , na majaribio matatu yaliyoshindwa, ikilinganishwa na utekaji nyara nne na majaribio 10 yaliyoshindwa mwaka 2010-2011, gazeti la Tanzania la The Guardian liliripoti hapo Jumanne (tarehe 17 Julai).

"Shughuli za uharamia zimepungua shukurani kwa vikosi vyetu vya majini," Nahodha alisema, na kuongeza kuwa serikali yake inazidisha uwezo wa jeshi katika kupambana na maharamia.

Waziri pia alisema kuwa hali ya kutokuwepo kwa utulivu katika nchi jirani bado ni wasi wasi mkubwa kwa Tanzania.

"Katika kipindi hiki, migogoro miongoni mwa baadhi ya nchi majirani zetu imechangia sana kuongezeka kwa matukio ya uhalifu na wahalifu nchini," Nahodha alisema. "Serikali imeiagiza Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa kutumia njia zake za kidiplomasia kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa migogoro."

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 9)

Dislike_icon(1)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo