Julai 13, 2012
Wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Afrika mjini Mogadishu wamefanikiwa kuyarudisha zaidi ya magunia 500 ya chakula kilichoibiwa kutoka kwenye kambi ya al-Shabaab iliyotekwa katika eneo la Laanta Buuro, ilisema taarifa ya AMISOM hapo Alhamis (tarehe 12 Julai).
Chakula hicho kilikuwa kimekusudiwa kwa msaada wa kibinaadamu, lakini al-Shabaab ilikuwa inakitumia kulisha wapiganaji wake katika kambi hiyo, umbali wa kilomita 40 magharibi ya Mogadishu. Chakula hicho sasa kimerudishwa kwa watu wa eneo hilo.
Wapiganaji 11 wa al-Shabaab waliuawa na wanne wakakamatwa mateka baada ya AMISOM kuichukua kambi hiyo hapo Jumatano, ilisema taarifa hiyo. AMISOM ilitangaza kwamba pia ilikamata rundo la silaha, zikiwemo bunduki na vifaa vya kutengenezea mabomu.
Kamanda wa AMISOM, Luteni Jenerali Andrew Gutti, alisema hivi karibuni mashirika ya misaada yataweza kuingia kwenye maeneo ambayo hadi karibuni yalizuia na al-Shabaab. "Tunatimiza wajibu wetu kusaidia utaratibu wa amani wa Somalia na kuandaa mazingira mazuri kwa ajili ya ufikishaji wa misaada ya kibinaadamu inayohitajika sana," alisema.
Wabunge wameondoa hoja yao inayomtaka Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon na baraza lake la mawaziri k...
Rais Ahmed Silanyo wa mkoa wa Somaliland alikutana na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya kwa Som...
Ukiritimba na ukosefu wa ufanisi katika bandari ya Dar es Salaam unaigharimu Tanzania na nchi jir...
Viongozi wa mkoa wa Puntland walikutana siku ya Jumanne (tarehe 21 Mei) kuwashajiisha wanawake ku...
Wanajeshi wa Somalia na wa Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) waliwakamata zaidi ...
Rais Ismail Omar Guelleh wa Djibouti alijadiliana ushirikiano wa kimkakati na Kanali Saleh Ben Na...
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, vikosi vya usalama na mahakama vinapaswa kuomba radhi hadharani kut...
Waziri Mkuu wa Djibouti Abdoulkader Kamil Mohamed alitoa wito wa kuongezwa kwa ushirikiano katika...
Baadhi ya wabunge wa Somalia wameitupilia mbali hoja ya kumtaka waziri mkuu na baraza lake la maw...
Wabunge wa upinzani walidai kwamba serikali ya Tanzania imekuwa ikibana uhuru wa kujieleza na kud...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji