Julai 12, 2012
Wafanyakaazi wawili wa misaada wa Kenya na daktari wa Kisomali walitekwa nyara huko Somalia siku ya Jumatano (tarehe 11 Julai), polisi walisema.
Utekaji nyara huo ulitokea karibu na mji wa Galkayo, unaogawa mpaka baina ya jimbo la kaskazini lenye serikali ya ndani na mkoa wa Galmudug.
"Wakenya wawili na daktari mmoja wa Kisomali walitekwa nyara na taarifa za mwanzo zinaashiria kuwa wateka nara walikuwa maharamia, lakini bado tunachunguza juu ya tukio hili," alisema Adan Warsame, afisa ndani ya polisi ya Galkayo, aliiambia AFP.
Mohammed Ise Hassan, afisa mwingine wa polisi, alisema dereva na walinzi wawili walijeruhiwa katika utekaji nyara huo.
Watu hao watatu waliotekwa nyara ni waajiriwa wa shirika lisilo la kiserikali la Sweden International Aid Services. Shirika hilo lilitoa taarifa nchi ya Uswidi ya kuthibitisha utekwaji nyara huo, lakini waliwataja wale waliotekwa kuwa ni wahamiaji watatu wa Kenya.
Huu ni utekaji nyara wa pili wa wafanyakazi wa misaada mwezi huu, kufuatiakutekwa kwa wafanyakazi wanne wa Baraza la Wakimbizi la Norwe. kutoka kmbi ya wakimbizi ya Dadaab nchini Kenya wiki iliyopita.
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi (tarehe 23 Mei) alitoa majina mawili ya mwisho ya ...
Watu watano waliuawa na wanne kujeruhiwa katika mashambulizi mawili kwenye eneo la kaskazini mash...
Sababu kuu ya vurugu ambazo ziliua zaidi ya watu 150 katika Delta ya Mto Tana mwaka jana ilitokan...
Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza mlipuko wa polio katika Pembe ya Afrika siku ya Jumatan...
Majeshi ya serikali ya Somalia yamezifungia kampuni za mawasiliano ya simu na biashara nyingine h...
Serikali ya Somalia itaanza kuunda tawala za kikanda katika maeneo yaliyokombolewa kutoka kwa al-...
Waziri wa Nishati wa Djibouti Ali Yacoub Mohamoud na Balozi wa Japani nchini Djibouti Atsushi Nis...
Ufunguzi wa Mkutano wa Wasambazaji wa mafuta na gesi Tanzania utafanyika huko Dar es Salaam tareh...
Wabunge wameondoa hoja yao inayomtaka Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon na baraza lake la mawaziri k...
Rais Ahmed Silanyo wa mkoa wa Somaliland alikutana na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya kwa Som...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji