Mkutano wa Bunge la Katiba ya Somalia waahirishwa

Julai 12, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Mkutano wa Bunge la Katiba ya Somalia, ambao ulipangwa kuanza siku ya Alhamisi (tarehe 12 Julai) mjini Mogadishu, umeahirishwa moja kwa moja.

Kuahirishwa huko kulikuja baada ya viongozi wa kikabila ambao wamekuwa wakikutana mjini Mogadishu kwa zaidi ya miezi mitatu iliyopita kushindwa kukidhi tarehe ya mwisho ya kuchagua wajumbe wa Bunge la Taifa la Katiba (NCA).

"Kuahirishwa huku ni matokeo ya kushindwa kwa makabila kuchagua wawakilishi wao kwa ajili ya Bunge la katiba," Mohammed Yakub, kiongozi wa kikabila mjini Mogadishu, aliiambia Sabahi. Alisema ni asili mia 60 ya NCA waliochaguliwa mpaka sasa.

Kwa mujibu wa ratiba iliyokubaliwa na viongozi wa kisiasa, iliamuliwa kuwa NCA lingeundwa tarehe 12 Julai ili kupitia na kuidhinishwa katiba mpya hapo tarehe 20 Julai, lakini viongozi wa kikabila wameshindwa kuipatia serikali majina 825 ya wajumbe.

Hii ni mara ya tatu kwa viongozi wa kikabila kupitiliza tarehe ya mwisho iliyowekwa ili kukamilisha kazi ya kuchagua wajumbe wa NCA. Hapo awali, viongozi wa kikabila walishindwa kuchagua wajumbe kwa ajili ya Bunge kabla ya tarehe 15 Mei , na kushindwa tena matakwa ya tarehe 20 Juni kuwa ni siku ya mwisho ya uteuzi wa bunge hilo.

Licha ya kuchelewa huko, Yakub alielezea imani yake kuwa viongozi wa kikabila wataweza kuchagua wajumbe waliobakia wa NCA kabla ya mwisho wa wiki hii.

"Mimi nina imani kubwa kuwa viongozi wa kikabila wataweza kukamilisha kazi hii nakutoa majina ya wajume wote wa Bunge la katiba ndani ya siku tatu zijazo," alisema. "Nina imani kubwa sana kuwa Mkutano wa Katiba utaanza siku ya Jumamosi tarehe 15 Julai."

Wakati unakimbia kwa viongozi wa Somalia ambao wanapaswa kumaliza kazi ya kuweka msingi ili kumaliza kipindi cha mpito ifikapo tarehe 20 Agosti. Kazi muhimu sana kati ya hizo ni kuidhinisha katiba mpya na kuchagua wabunge wa bunge jipya si zaidi ya tarehe 20 Julai.

Katika siku za karibuni zilizopita, Raisi Sheikh Sharif Sheikh Ahmed na Waziri Mkuu Abdiweli Mohamed Aliwamefanya mfulilizo wa mikutano na viongozi wa kikabila ili kuwahamasisha kukaza hatua katika kuchagua wajumbe wa NCA, wakati viongozi hao wa kikabila wakidadi kutaka muda zaidi wa kuijadili rasimu ya katiba kabla ya kuunda bunge hilo.

Ali alisema katiba ni waraka halali na sekta zote za jamii ya Somalia zitaingizwa katika NCA.

"Tunakaribia kufika tarehe ya mwisho na tunawajibika kwa jamii yenye amani na demokrasia," Ali alisema katika maelezo hapo Jumanne, kwa mujibu wa Radio Kulmiye.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo