Tanzania yakazania mahitaji ya kutoa ripoti kwa mpango wa Benki ya Dunia

Julai 08, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Wizara ya Kilimo, Usalama wa Chakula na Ushirika ya Tanzania, imeanzisha mpango wa utoaji risiti kwa wasambazaji wa mahitaji ya kilimo unaofanyakazi chini ya Sekta ya Mpango wa Maendeleo ya Kilimo (ASDP), gazeti la Tanzania la Daily News liliripoti hapo Jumapili (tarehe 8 Julai).

Wasambazaji wa mahitaji ya kilimo kama vile mbolea, mbegu bora na wataalamu wa ushauri sasa watahitajika kuwasilisha risiti kwa vitu walivyonunua kwa ajili ya usambazaji, kwa Maafisa Kilimo na Ufugaji wa Wilaya (DALDO) kabla ya kuwepa fedha zao, kwa mujibu wa afisa mkuu wa wizara, Michael Mayabu. Mahitaji ya risiti ni kwa ajili ya uchunguzi wa kiusalama, alisema.

Mayabu aliwaonya maafisa wa DALDO dhidi ya kuwalipa wasambazaji ambao watashindwa kuwasilisha risiti. "Ikiwa mtawalipa bila ya kupokea risiti kwanza mjue mnafanya hivyo kwa maamuzi na hasara yenu, kwa sababu ni kinyume na taratibu," alionya.

ASDP imekuwa ikifanyakazi kwa zaidi ya miaka mitatu, na imesaidia kupatikana mazao ya mahindi na mpunga mara mbili au tatu kwa kila hekta moja katika wilaya ambazo mpango huo unafanyakazi, alisema afisa mkuu wa wizara anayeshughulikia kilimo, Sarah Mlay.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo