Jeshi la Kenya laanza kuandikisha askari wahitimu katika sayansi, na teknolojia

Julai 08, 2012

  • 3 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Vikosi vya Ulinzi vya Kenya vyatafuta kuandikisha askari wahitimu wa chuo kikuu pamoja na kuwapa mafunzo katika nyuga za kiufundi, gazeti la Kenya la Daily Nation liliripoti Jumamosi (tarehe 7 Julai).

Wataalamu wa kuandikisha askari katika maeneo kama vile maendeleo ya programu za kompyuta, mifumo ya taarifa za kijiografia na mambo ya hali ya hewa ni sehemu ya programu za kisasa zilizobuniwa kufanya vikosi hivi kuwa na ufanisi zaidi," alisema msemaji wa jeshi meja Emmanuel Chirchir. "Kama ilivyo kwenye taasisi zozote, kuna vipengele vya taarifa vinavyotakiwa katika operesheni za kisasa."

Kapteni mstaafu Simiyu Werunga alisema vikosi vyenye mafunzo makubwa vitakidhi mahitaji ya jeshi kutengeneza ramani zenye taarifa za kina kuhusu ardhi ya mapigano, kutabiri ruwaza za hali ya hewa na silaha za kisasa.

Vikosi vya Kenya vinavyopambana na al-Shabaab nchini Somalia sasa viko rasmi chini ya mwamvuli wa Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 3)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • kelvin Njaramba
    June 17, 2013 @ 03:53:10AM

    Ninamuomba Mungu alilinde jeshi.

  • simon ngugi karanja
    May 21, 2013 @ 05:11:35AM

    MIMI NI RAIA WA KENYA MWENYE UMRI WA MIAKA 25 SASA. Kwa upande wa sayansi na teknolojia ndio ninaofanya vizuri. Tayari nmeshamaliza kozi ya uhandisi wa ndege katika chuo cha uendeshaji ndege cha shirika la ndege la Trans-eastern Airline kilichoko Bomas of Kenya, na nimepata alama ya kufaulu katika mtihani wangu wa KNEC. Ninao uzoefu wa kazi katika ndege za kiraia usiopungua mwaka mmoja. Pia ninaweza kufanya mradi kama vile mfumo wa kudhibiti kifaa kwa mbali. Nikipewa kazi ninaweza kuonesha kwa vitendo kipaji nilichonacho katika sayansi na teknolojia. Shukrani mapema.

  • kxodo
    July 9, 2012 @ 07:45:55AM

    Ni vyema kutumia intelijensia katika vikosi, ambapo ninajidai nilikuwemo humo kabla. Inakuwaje sasa Kabuga bado inalindwa na vikosi vyetu na tunaweza kuona vipi washirika wako huko DRC walilazimishwa kurudi nyuma? Wakati kondoo anayelindwa inasemekana kuwa na mkono katika vikosi vya waasi?

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, serikali za majimbo ya shirikisho ziundwe vipi nchini Somalia kufuatia utata wa Jubbaland?

Angalia matokeo