Wakuu wa juu wa usalama wahamishwa baada ya mashambulizi ya makanisa huko Garissa

Julai 06, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Ofisi ya raisi ya Kenya imetangaza uhamisho wa maafisa wakuu wa usalama katika Mkoa wa Kaskazini Mashariki mwa Kenya siku ya Alhamisi (tarehe 5 Julai), siku nne baada ya mashambulizi ya makanisa mawili huko Garissa yaliyoua watu 17 na kujeruhi makumi ya watu.

Kaimu Waziri wa Usalama wa Ndani Yusuf Hajji na Kamishna wa Polisi Mathew Iteere waliwaambia waandishi wa habari mjini Nairobi kuwa hatua hiyo inakusudia kushughulikia masuala ya kutokuwepo kwa usalama baada ya watu wenye silaha kulishambulia kwa maguruneti na bunduki Kanisa la African Inland na Kanisa Kuu la Kikatoliki.

Vilevile, Hajji alisema maafisa usalama 700 watapelekwa katika mkoa huo kusimamia vitisho vya al-Shabaab.

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Mashariki James ole Seriani atahamishiwa Mkoa wa Magharibi akiwa na cheo hicho hicho, na nafasi yake kuchukuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani wa zamani Ernest Munyi.

Mabadiliko haya pia yanawahusu idadi kubwa ya wakuu wa wilaya na maafisa wa polisi.

Seriani aliwataka wakazi katika eneo hilo kusaidia na kushirikiana na wakuu wapya wanaokuja ili kupambana na hali ya kutokuwepo kwa usalama.

Alisema kuwa mashambulizi ya makanisa yalikuwa ni tukio la bahati mbaya sana katika miaka yake mitatu kama mkuu wa mkoa huo. "Shambulio limeonesha kuwa magaidi hawaheshimu sehemu za ibada na raia na kwamba kila mtu lazima awe angalifu ili kuzuia mauaji ya kinyama ya watu wengi kama hao," Seriani aliiambia Sabahi.

Hata hivyo, Seriani alisema kuwa anahakikia kuwa vita na al-Shabaab nchini Kenya na Somalia vitashinda. "Wakati wa muda wangu katika mkoa huu, tuliawana changamoto na mafanikio mengi. Nilijaribu kutimiza maadili ninayoyapenda -- kama kupambana na ugaidi na unyang'anyi, na kufahamu mustakabali wa wachungaji. Ulikuwa heshima," alisema.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 3)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo

Nyenzo