Julai 05, 2012
Polisi ya Kenya imewakamata zaidi ya washukiwa 30 kuhusiana na mashambulizi ya makanisa mawili huko Garissa mwishoni mwa wiki iliyopita, yaliyoua kiasi cha watu 16 na kujeruhi kwa makumi, Radio Capital FM ya Kenya iliripoti hapo Jumatano (tarehe 4 Julai).
"Tumekuwa tukichukua hatua kali na tumewakamata washukiwa kadhaa ambao wanahojiwa," alisema Naibu wa Polisi wa Mkoa wa Kaszini Mashariki Phillip Ndolo.
Kiasi cha washukiwa 20 wako kizuizini kwa mahojiano zaidi, wakati wengine waliachiwa huru kwa kukosekana ushaidi wa kutosha, CCN ilimnukuu Ndolo akisema.
Kaimu Waziri wa Usalama wa Ndani Yusuf Haji alisema maafisa 700 wa ziada wamepelekwa mjini kote na wanazunguka maeneo ili kudhibiti vitisho vya kutokuwepo na usalama kutoka kwa al-Shabaab, Capital FM iliripoti.
"Tumefanya matayarisho maalumu katika kuweka usalama na hii inajumuisha wafanyakazi zaidi wa usalama waliosambazwa," Haji alisema hapo Alhamis.
Wakati huo huo, viongozi wa Kiislamu wamesema watasaidia kuyalinda makanisa wakati wa sala, BBC iliripoti.
"Tuliamua kama hatua ya mshikamano vijana wa Kiislamu watatoa huduma za ulinzi makanisani sio tu kwa Garissa, lakini katika maeneo mengine yoyote ambako Wakristo watahisi inafaa," alisema Adan Wachu, mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Kenya na Baraza la Dini la Kenya.
"Haitaruhusiwa kuwa na mgawanyiko wa vikundi kama huo ndani ya nchi yetu -- yeyote atakayefanya hivyo bila shaka atashindwa," alisema.
Wabunge wameondoa hoja yao inayomtaka Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon na baraza lake la mawaziri k...
Rais Ahmed Silanyo wa mkoa wa Somaliland alikutana na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya kwa Som...
Ukiritimba na ukosefu wa ufanisi katika bandari ya Dar es Salaam unaigharimu Tanzania na nchi jir...
Viongozi wa mkoa wa Puntland walikutana siku ya Jumanne (tarehe 21 Mei) kuwashajiisha wanawake ku...
Wanajeshi wa Somalia na wa Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) waliwakamata zaidi ...
Rais Ismail Omar Guelleh wa Djibouti alijadiliana ushirikiano wa kimkakati na Kanali Saleh Ben Na...
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, vikosi vya usalama na mahakama vinapaswa kuomba radhi hadharani kut...
Waziri Mkuu wa Djibouti Abdoulkader Kamil Mohamed alitoa wito wa kuongezwa kwa ushirikiano katika...
Baadhi ya wabunge wa Somalia wameitupilia mbali hoja ya kumtaka waziri mkuu na baraza lake la maw...
Wabunge wa upinzani walidai kwamba serikali ya Tanzania imekuwa ikibana uhuru wa kujieleza na kud...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji