Julai 03, 2012
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na ushirika wa taaisi nane za fedha wamesaini makubaliano ya mkopo wa shilingi bilioni 165 (Dola za Kimarekani milioni 104) kwa ajili ya kujenga nyumba za bei nafuu siku ya Jumatatu (tarehe 2 Julai), gazeti la Daily News la Tanzania liliripoti.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ya Watu, Anna Tibaijuka alisema mkataba huu "ni mkubwa kuliko yote iliyowahi kutolewa ya kuendeleza makazi nchini Tanzania".
Jumla ya benki saba za ndani, mifuko ya kijamii na taasisi nyingine za fedha ilichangia fedha katika mkopo huo.
NHC limepanga lengo la uchangiaji wa awali wa shilingi bilioni 310 (Dola za Kimarekeni milioni 196) kutekeleza mpango mkakati wake wa 2010-2015, lakini awamu hii ya kwanza italiwezesha shirika hilo la serikali kufikia lengo lake la kujenga nyumba 15,000 kabla ya mwaka 2015, alisema Mkurugenzi mkuu wa NHC Nehemia Mchechu.
Wizara ya Usafiri wa Anga ya mkoa wa Somaliland siku ya Jumanne (tarehe 18 Juni) iliikataza ndege...
Polisi nchini Tanzania waliwakamata makamu wanne wa chama kikuu cha upinzani cha Demokrasia na Ma...
Watu wenye silaha kwenye Kaunti ya Wajir walimuua polisi mmoja wa akiba wa Kenya siku ya Jumanne ...
Japan inaipa Tanzania dola milioni 49 (shilingi bilioni 80.4) kama msaada na mkopo kwa ajili ya k...
Inspekta Jenerali wa Polisi David Kimaiyo yeye pekee yake amewateua na kuwapangia kazi maafisa wa...
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) siku ya Jumanne ilimkubalia Makamu wa Rais wa Kenya Willia...
Polisi waliwakamata mamia ya watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa al-Shabaab katika wilaya za Hod...
Kongamano la siku tatu juu ya elimu lilifunguliwa mjini Mogadishu siku ya Jumanne (tarehe 18 Juni...
Wanajeshi wa serikali ya Somalia wakisaidiwa na wanajeshi wa Misheni wa Umoja wa Mataifa (AMISOM)...
Waziri wa Mambo ya Ndani na Uratibu wa Serikali ya Kitaifa, Joseph Ole Lenku, siku ya Jumatatu (t...
(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji
Maoni ya msomaji
Napenda kujua hizi nyumba za bei nafuu ni kwa watumishi tu au?,na kama ni kwa watumishi ni utaratibu upi unatumika kumfikia muhitaji kwa wakati?,na je muhitaji anaweza kuhudumiwa popote pale Tanzania?.Kama sawa Vigezo tafadhali
ningependa kujua kua hizo nyumba za bei nafuu naweza kujengewa mahali ninapopataka mimi.