Hospitali ya Kenya yatoa ombi la wachangiaji damu kwa waathirika katika kanisa huko Garissa.

Julai 03, 2012

  • 1 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Hospitali ya Taifa ya Kenyatta imetoa ombi la kuongezeka kwa uchangiaji damu kuokoa maisha ya waathirika sita ambao walipata majeraha makubwa Jumapili katika mashambulio ya kanisa huko Garissa, gazeti la Kenya la The Standard liliripoti Jumatatu (tarehe 2 Julai).

Hospitali hiyo iinawapatia matibabu waathirika saba wa mashambulio ya Jumapili -- wanawake wanne na wanaume watatu. Si chini ya watu sita waliuawa katika shambulio hilo, na dazeni walijeruhiwa.

"Tunahitaji damu kwa haraka kwakuwa wagonjwa sita wanatakiwa kufanyiwa operesheni," alisema Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo Richard Lesiyampe. "Tunatoa wito kwa Wakenya kujitokeza na kuchangia damu kusaidia raia wenzao.

"Tunafanya kila linalowezekana kurejesha afya ya wagonjwa hawa," Lesiyampe alisema.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • anita
    July 4, 2012 @ 06:17:20AM

    Sheria mpya ya ugaidi lazima iimarishwe. Magaidi wasiachiwe kwa dhamana na washitakiwe kama wauwaji. Fikiria watu 17 wameuawa, na wakati magaidi wanapokamatwa, wanaachiwa kwa dhamana na mwisho wanarejea kufanya ugaidi kwa watu wa Kenya wasio na hatia. Lazima sheria ipitiwe na kupewa kipaumbele cha mwanzo katika bunge letu.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo

Nyenzo