Wafanyakazi wa msaada waliookolewa wawasili nchini Kenya

Julai 03, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Wafanyakazi wa misaada wanne waliotekwa nyara kutoka katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab Ijumaa waliwasili Nairobi siku ya Jumatatu (tarehe 2 Julai) baada ya kukombolewa kutoka kwa watekaji wao nchini Somalia, AFP iliripoti.

  • Wafanyakazi wa misaada wageni wanne waliotekwa nyara katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab nchini  Kenya Ijumaa wakiwa wanatabasamu wakati walipowasili kwa usalama jijini Nairobi Jumatatu (tarehe 2 Julai), Tony Karumba/AFP.

    Wafanyakazi wa misaada wageni wanne waliotekwa nyara katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab nchini Kenya Ijumaa wakiwa wanatabasamu wakati walipowasili kwa usalama jijini Nairobi Jumatatu (tarehe 2 Julai), Tony Karumba/AFP.

"Tunafurahi kuwa hai. Tunafurahi haya yamekwisha," alisema Quarat-UI-Ain Sadazai, Mkanada mwenye asili ya Pakstani na mmoja wa wafanyakazi waliotekwa wa Baraza la Wakimbizi la Norwe (NRC).

Sadazai, mwenye umri wa miaka 38, na wenzake -- Steven Dennis, mwenye umri wa miaka 37, ambaye pia ni Mkanada; Astrid Sehl, mwenye umri wa miaka 33, Mnorwe; na Glenn Costes, mwenye umri wa miaka 40, wa Ufilipino -- waliokolewa na kikosi cha pamoja cha Somalia na vikosi vya Kenya baada ya mapigano ya silaha ya muda mfupi ambapo mmoja wa watekaji aliuawa na washukiwa watatu walikamatwa.

Shukrani ni kwa Mungu tulizuia malengo yao ya kuwachukua mateka hawa na kuwapeleka msituni," alisema Jenerali wa Somalia Osmail Sahardid, ambaye aliongoza operesheni hiyo.

Isipokuwa kwa mtuti wa bunduki tuliweza kuwaokoa, kundi hili liliwasili Nairobi bila kudhurika.

"Tunashukuru sana kujua kuwa wenzetu wanne walipatikana na walirudishwa Kenya kwa usalama. Hii ni siku ya faraja kwetu na kwa familia za watekwaji," alisema katibu Mkuu wa NRC Elizaberth Rasmusson.

Fikra zetu za pole ziendee familia ya dereva wa NRC Abdi Ali, ambaye aliuawa wakati wa shambulio hilo Ijumaa na wafanyakzi wawili wa ndani ambao kwa sasa wanapata matibabu katika hospitali kwa majeraha yaliyotokana na tukio hilo. alisema.

Mseamaji wa NRC Rolf Vestvick alisema shirika hilo lilipunguza operesheni zake huko Dadaab mwishoni mwa wiki, lakini halitaondoa kabisa jitihada zake za misaada. "Tunamatumaini kuwa tutaweza kuendeleza kazi zetu," aliiambia televisheni ya CTV News Channel.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 2)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo