Kenya yaondosha madai ya ugaidi kwa Mjodani

Julai 02, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Waendesha mashitaka wa Kenya wameondosha madai ya ugaidi dhidi ya raia wa Jordan mwenye hati za ukimbizi nchini Uswisi, maafisa wa polisi walisema hapo Jumatatu (tarehe 2 Julai).

"Mashitaka yote, ukiachia kuwemo nchini isivyo halali, yametupiliwa mbali na upande wa mashitaka kutoka na kukosekana ushahidi wa kutosha," makamo msemaji wa polisi Charles owino aliiambia AFP.

Magd Najjar, mwenye umri wa miaka 19, alishikiliwa na polisi baada ya kuingia nchi isivyo halali mwezi Mei. Alishitakiwa katika mahakama ya Nairobi hapo tarehe 6 Juni kwa "kujihusisha na vitendo vya uhalifu wa kupangwa kwa kuwa mwanachama wa al-Shabaab, kikundi cha kihalifu kilichopigwa marufuku."

Mwishoni mwa wiki Uswisi ilisema ilimkatalia Najjar kurejea nchini huko, kwa kuonyesha kuwa angeweza kukosa hadhi yake ya ukimbizi kutokana na tukio hilo.

Owino alisema kuwa Najjar alilipa faini na kuachiliwa, lakini hakusema kwa sasa yuko wapi.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 0)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo

Nyenzo