Rais wa Somalia atembelea Balad iliyokombolewa hivi karibuni

Julai 01, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Raisi wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed alitembelea mji wa Balad uliokombolewa hivi karibuni Jumamosi (tarehe 30 Juni).

Hadi sasa wakati wa ziara yake, Ahmed alikagua vituo vya kijeshi kadhaa na majengo yaliyochakaa katika mji wa Shabelle ya Kati baada ya vikosi vya AMISOM na Somalia kuukomboa kutoka kwa al-Shabaab Jumanne, Redio RBC ya Somalia iliripoti.

Ahmed alivisifu vikosi vya Umoja wa Afrika na vya serikali ya Mpito ya Shirikisho ya Somalia, na kuapa kuendeleza mapigano katika nchi yote dhidi ya al-Shabaab hadi watakapotoweka kabisa nchini Somalia.

“Serikali inajaribu kudumisha sheria na amri katika maeneo yaliyokombolewa upya na tunatarajia kupata msaada kutoka kwa watu wa ndani,” alisema. “Hatutaruhusu nafasi yeyote isiyo ya usalama kutokea kwa sababu tunajua kuwa baadhi ya waharibifu wanaweza kutaka kutumia hali kama ya wakati huu.”

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 1)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo