Mahakama yaongeza muda wa kuwekwa kizuizini kwa washukiwa wa bomu

Juni 29, 2012

  • + Toa maoni sasa
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Mahakama ya Mombasa imetoa ruhusa kwa polisi kumshikilia mtu anayeshukiwa kwa upigaji bomu Jumapili iliyopita huko Mombasa kwa siku 10 zaidi, gazeti la Daily Nation la Kenya liliripoti Alhamisi (tarehe 28 Juni).

Mtuhumiwa huyo, Athuman Salim Kassim, amekuwa kizuizini tangu shambulio la tarehe 24 Juni na atatolewa kutoka hospital na kupelekwa kituo cha polisi.

Inspekta Mkuu wa Polisi Luka Tumbo alisema katika hati ya kiapo kuwa anazo taarifa zinazoonyesha uhusiano wa Kassim na upigaji bomu katika bar, ambapo watu watatu waliuawa na 30 kujeruhiwa.

Pia siku ya Alhamisi, Naibu Waziri Mkuu Musalia Mudavadi aliwataka polisi kuanzisha uchunguzi katika shambulio la Mombasa. “Tunawataka polisi kuanzisha uchunguzi wa kina na kuwakamata watu waliohusika na mlipuko ambao ulisababisha vifo kadhaa na kuwajeruhi wengine,” alisema.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 2)

Dislike_icon(0)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo