Viongozi wa Kiislamu wataka mabadiliko katika sheria Kenya dhidi ya ugaidi

Juni 29, 2012

  • 1 Maoni
  • Chapisha
  • Panga upya Punguza Ongeza

Jumuiya ya Uongozi wa Waislamu wa Kenya imeomba mabadiliko kadhaa katika Mushwada wa Kujilinda na Ugaidi ya mwaka 2012 kabla ya kutiwa saini, Redio ya Capital News FM ya Kenya iliripoti hapo Alhamisi (tarehe 28 Juni).

Viongozi wa jumuiya hiyo wanasema wanataka kuwalinda Waislamu kutokana na bughudha na kubaguliwa, na kuhakikisha kuwa vikosi vya usalama haviwasumbui watu kwa jina la kupigana na ugaidi.

“Tendo lolote linalowasumbua watu au sehemu ya umma linachukuliwa kama tendo la ugaidi, ni maoni yetu kuwa ufafanuzi ifasiliwe (tena) na kuongeza vitendo maalum,” alisema Mkurugenzi Mkuu Fazul Mahamed katika taarifa yake kwa Waziri wa Usalama wa Ndani.

Kikundi cha viongozi wa Kiislamu pia wanataka muswada huo kuhakikisha haki za binadamu za washutumiwa wa ugaidi nchini. “Wahutumiwa lazima wahakikishiwe uwakilishi. Kusiwe na haki yao yoyote ya msingi itakayo vunjwa,” Mahamed alisema.

Taarifa ya Mahamed inakusudia kupingana na ile ya Jumatatu, ambapo mwenyekiti Sheikh Fazul Mahamed Mponda aliposema jumuiya iliupitia muswada na inauunga mkono kikamilifu.

Waziri Mkuu wa Wizara ya Usalama wa Ndani Mutea Iringo alikubaliana na wasi wasi wao. Lakini alisema katiba ya Kenya tayari inayashughulikia baadhi yao, ikiwa ni pamoja na huduma ifaayo kwa wasshukiwa wakiwa wameshikiliwa na polisi. Katika muswada huo mpya wa sheria, washutumiwa hawawezi kutendewa vibaya na polisi au kuwekwa kizuizini kwa zaidi ya saa 24, isipokuwa iwe imeelekezwa na mahakama ya sheria.

Pia katika sheria hiyo mpya, yeyote atayeshitakiwa kwa kutenda ugaidi utakaosababisha vifo anaweza kufungwa kifungo cha maisha.

Muswada wa Kujilinda na Ugaidi ya 2012 ililetwa kwa mara ya kwanza mwaka 2003 na baadaye kuondoshwa baada ya madai ya ukosoaji kutoka kwa baadhi ya vikundi vya Waislamu.

Unaonaje kuhusu makala hii? (Jumla ya Kura 5)

Dislike_icon(3)

(Sera za kutoa Maoni) *Inaonesha Maeneo yanayohitaji

Maoni ya msomaji

  • yusuf abdallah
    August 27, 2012 @ 06:23:08AM

    Mswada wa sheria uliondolewa kutokana na shinikizo la vikundi nchini Kenya kote, na kusema tu kuwa Waislamu inapotosha. Baada ya katiba mpya sheria zote za kushughulikia uhalifu upo na tunapaswa tuweke sheria mpya kama inavyofanywa kwa ajili ya ugaidi. Cha kufanya ni kuunda timu ambayo itashughulikia masuala ya ugaidi ili katiba iwe imewakilshwa vyema.

Habari Mpya kabisa

Katika Mwangaza

Jisajili

Kura

Je, unadhania kupigwa marufuku kwa hotuba ya chuki na Tanzania kutakomesha mashambulizi dhidi ya makanisa na misikiti?

Angalia matokeo